Asia Pasifiki

IAEA inaripoti matumaini kuhusu mazungumzo ya Iran-Marekani, na wasiwasi kufuatia majaribio ya kinyuklia ya DPRK

Ripoti ya Mkuu wa Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Kinyuklia (IAEA), Mohamed ElBaradei iliowakilishwa kwenye Bodi la Magavana, imebainisha kuwa na matumaini ya kutia moyo, katika kuanzisha mazungumzo baina ya Teheran na Washington, kuzingatia masuala ya miradi ya kinyuklia inayoendelezwa na Iran hivi sasa pamoja na mada nyeginezo.

Nusu ya vifo vya barabarani huathiri wenda kwa miguu, wapanda baiskeli na wanaoendesha motosekli/pikipiki

Utafiti mpya uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) umethibitisha ya kuwa nusu ya watu milioni 1.27 wanaokadiriwa kufariki kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, ni watu wanaokwenda kwa miguu, na wale wanaopanda baiskeli na wanaoendesha motosekli/pikipiki.

Uongozi mpya unahitajika kukabiliana na mizozo ya ajira duniani. inasema ILO

Juan Somavia, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) alipohutubia kikao cha ufunguzi wa Mkutano Mkuu juu ya Masuala ya Mizozo ya Ajira Duniani, uliofanyika Geneva, amependekeza kuwepo “uongozi mpya katika viwango vyote vya kiuchumi na kijamii" ili kusuluhisha vyema mizozo ya ajira kimataifa. Mkuu huyo wa ILO, alisema ulimwengu hauwezi tena kusubiri uchumi ukuwe, kwanza, kwa miaka kadha kabla ya kuamua kuzalisha ajira.

Mkuu wa WHO ahimiza haki kwenye sera za kimataifa

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dktr Margaret Chan aliwaambia wajumbe wa kimataifa, waliohudhuria warsha maalumu uliofanyika Makao Makuu ya UM, kuwacha ile tabia ya “kuamini, bila kuelewa, madai yanayojigamba ustawi wa uchumi na natija zake kimataifa ndio mambo yatakayofanikiwa kumaliza na kuponya matatizo yote ya maisha duniani.”

Ulimwengu sasa umo kwenye mkumbo wa awali wa maambukizo ya janga la homa ya A(H1N1), yahadharisha WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) wiki hii limepandisha kiwango cha tahadhari ya maambukizi ya homa ya mafua ya aina ya A(H1N1) kutoka daraja ya 5 mpaka ya sita.

Siku ya Dunia Dhidi ya Ajira ya Watoto Wadogo

Kwenye kumbukumbu ya miaka 10 ya Siku ya Dunia dhidi ya Ajira ya Watoto wa Umri Mdogo, siku ambayo huadhimishwa tarehe ya leo kulitolewa mwito maalumu na Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF), likijumuika na mashirika wenzi wa kuhimiza jamii ya kimataifa kukabiliana na sababu za msingi zenye kuchochea umasikini na ufukara, hali ambayo inaaminika ndio yenye kuwalazimisha watoto wenye umri mdogo kutafuta ajira ya kumudu maisha.

Maendeleo kupatikana kwenye mkutano wa kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa

Mkutano wa UM uliofanyika Bonn, Ujerumani mwezi huu, kuzingatia masuala yanayohusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani, umemalizika Ijumaa ya leo na iliripotiwa kumepatikana mafanikio ya kuridhisha katika maandalizi ya waraka wa ajenda ya majadiliano, kwa kubainisha dhahiri matarajio ya serikali wanachama kutoka Mkutano ujao wa Copenhagen, ili kuharakisha udhibiti bora wa taathira za mabadiliko ya hali ya hewa kimataifa.

BU laamrisha vikwazo ziada dhidi ya DPRK

Baraza la Usalama limekutana leo adhuhuri, na kupitisha, kwa kauli moja, azimio 1874 (2009) liliopendekeza kuchukuliwa hatua kali za kuweka vikwazo dhidi ya miradi ya kutengeneza silaha za kinyuklia na makombora katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea/Korea ya Kaskazini (DPRK).

Homa ya mafua ya A(H1N1) yatambuliwa na WHO kuwa janga la ugonjwa wa kuenea kimataifa

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza ilani maalumu yenye kuthibitisha kwamba Homa ya Mafua ya A(H1N1) sasa inatambuliwa rasmi kuwa ni janga la ugonjwa wa kuenea kimataifa - hii ni aina ya ilani ambayo inatangazwa tena kwa mara ya kwanza na WHO baada ya kipindi cha miaka 40.

UNAIDS kuuzindua umma wa kimataifa, VVU ni washiriki bubu wa maafa ya dharura

Mumtaz Mia, mshauri wa Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya UKIMWI (UNAIDS) kwa ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, amenakiliwa akitahadharisha ya kwamba mara nyingi, hasakatika mataifa yanayoendelea, huduma ya kuzuia maambukizo ya virusi vya UKIMWI huwa haipewi umuhimu unaostahiki, hasa baada ya kuzuka mizozo kadhaa ya dharura katika majiraya karibuni.