Asia Pasifiki

Kuondoka kwenye makaa ya mawe 'haitakuwa rahisi' lakini ni muhimu, asema Naibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Naibu katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J Mohammed ametoa wito kwa mataifa ya Barani Asia na Pasifiki kuharakisha kuacha kutumia mafuta ya Kisukuku na badala yake watumie nishati zenye kutoa kaboni kiasi cha chini ili kulinda mazingira na pia ikiwa ni njia mojawapo ya kuleta haki na ujumuishi.

Guterres aunga mkono maandalizi ya azimio la kupinga vilipuzi

Huko Geneva, Uswisi kuanzia tarehe 6 hadi 8 ya mwezi ujao wa Aprili kunafanyika mashauriano yasiyo rasmi yenye lengo la kuandaa azimio la kisiasa la kulinda raia dhidi ya matumizi ya vilipuzi katika maeneo ya makazi ya watu wengi.

Tujifunze kwa yaliyopita, tushikamane kutokomeza ubaguzi wa rangi:Guterres 

 Hii leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kumbukizi ya waathirika na manusura wa biashara ya utumwa katika bahari ya Atlantiki Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “kuna mengi tunayofahamu kuhusu biashara hiyo na leo ni siku ya kukumbuka uhalifu dhidi ya binadamu, usafirishaji na biashara haramu ya binadamu pamoja na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu usioweza hata kuzungumzika.”  

Tuwekeze kwenye tafiti na matibabu ya TB kunusuru kizazi cha sasa na kijacho - WHO

Ikiwa leo ni Siku ya kifua kikuu duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limetoa wito kwa serikali na wadau kuongeza uwekezaji katika huduma za Kifua Kikuu na utafiti hususan kwa watoto na vijana. 

Mkurugenzi Mkuu Mpya wa ILO kujulikana leo

Hivi sasa wajumbe wa Baraza la uongozi la shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani ILO wanapiga kura ya siri kuchagua mkurugenzi mkuu mpya ambaye atatangazwa punde baada ya uchaguzi kukamilika .

Kila mtu anapaswa kulindwa kwa tahadhari ya mapema dhidi ya majanga:UN 

Ikiwa leo ni siku ya utabiri wa hali ya hewa duniani, malengo mapya ya Umoja wa Mataifa yalioyotangazwa leo yanataka katika miaka mitano ijayo kila mtu kote duniani alindwe kwa kupewa tahadhari ya mapema dhidi ya ongezeko la hali mbaya ya hewa na mabadiliko ya tabianchi. 

Tunatembea tukiwa usingizini wakati wa kukabili  uchafuzi wa hali ya hewa: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema wakati mabishano baina ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea yakiendelea juu ya uchafuzi wa tabaka la ozoni na nani amefanya nini katika kupunguza uchafuzi huo, hali ya hewa inazidi kuwa mbaya na joto likizidi kuongezeka duniani kote.

Ni wakati wa kuhakikisha usimamizi bora na endelevu wa misitu:Guterres

Misitu bora ni muhimu kwa ajili ya watu na sayari dunia amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya misitu hii leo.  

Ubaguzi rangi watia sumu kwenye taasisi na jamii - Guterres

Ubaguzi umeendelea kutia sumu kwenye taasisi, miundo ya kijamii na katika maisha ya kila siku, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo wakati wa mkutano maalum wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliofanyika jijini New York, Marekani juu ya kile kinachoitwa kuwa kichocheo cha kuhalalisha chuki, kupinga utu na kusambaza ghasia.
 

Chonde chonde Uingereza fikirieni upya mswada wa sheria ya uhamiaji:UN

Umoja wa Mataifa umeisihi serikali ya Uingereza na watunga sheria kufikiria upya juu ya mswada wa  sheria mpya ya Utaifa na mipaka ya nchi hiyo kwakuwa ikipitishwa kama iliyo itakuwa na athari kubwa kwa wahamiaji na wakimbizi. Flora Nducha ana taarifa zaidi .