Kikao cha pili cha Kamati ya Utafiti wa Kisayansi, kilichoongozwa kimataifa kutokea ofisi za UM za Geneva, leo jioni, kilikusanyisha wanasayansi na matabibu 150, kutoka sehemu mbalimbali za dunia, ambao walishauriana, kwa kutumia njia ya vidio, masuala kadha wa kadha kuhusu utaratibu unaofaa kuchukuliwa kidharura kutengeneza chanjo ya kudhibiti vimelea vya homa ya mafua ya A(H1N1), na kuzingatia kiwango halisi cha maambukizi ya maradhi duniani kwa sasa.