Asia Pasifiki

Mkutano wa BK kuzingatia matatizo ya uchumi na fedha duniani waakhirishwa

Ijumanne asubuhi, kwenye kikao cha wawakilishi wote wa Baraza Kuu (BK) la UM, kulichukuliwa uamuzi wa pamoja wa kuakhirisha Mkutano Mkuu juu ya Migogoro ya Uchumi na Fedha Duniani na Athari Zake Dhidi ya Maendeleo, kikao ambacho kilitarajiwa kifanyike baina ya Juni 1 hadi 03.

Majaribio ya DPRK kuripua bomu la nyuklia chini ya ardhi yalaumiwa kimataifa

Baraza la Usalama, Ijumatatu jioni, baada ya kumaliza kikao cha faragha, lilipitisha Taarifa ya Raisi kuwakilishwa mbele ya waandishi habari wa kimataifa na Balozi Vitaly Churkin wa Shirikisho la Urusi, aliye raisi wa Baraza kwa mezi Mei.

Mazungumzo juu ya kikao cha mwaka kuhusu wenyeji wa asili

Kuanzia wiki iiliopita, kwenye Makao Makuu ya UM, kulikusanyika wajumbe karibu 2,000, waliowakilisha mashirika kadha wa kadha, ya wenyeji wa asili waliotokea sehemu mbalimbali za dunia, ambao walihudhuria kikao cha mwaka, cha wiki mbili, kuzingatia taratibu za kuchukuliwa kimataifa, kutekeleza mapendekezo ya ule Mwito wa UM juu ya Haki za Wenyeji wa Asili.

Siku ya Kimataifa Kuhishimu Viumbe Hai Anuwai

Tarehe ya leo, 22 Mei (2009) ni mwezi unaodhamishwa kila mwaka na UM kama ni Siku Kuu ya Kimataifa ya Kuhishimu Viumbe Hai Anuwai.

Baraza la WHO lahitimisha mkutano wa mwaka Geneva

Mkutano wa mwaka wa Baraza Kuu la Shirika la Afya Duniani (WHO) umemaliza kikao cha 2009 Ijumaa ya leo, kikao ambacho Mkurugenzi wa WHO, Dktr Margaret Chan alisema kilifanikiwa kuwapatia walimwengu “bishara ya nguvu ya masharti ya kudumu kuhusu maamirisho ya miradi ya afya ya jamii” pote ulimwenguni.

Nchi zinazoendelea zahitajia misaada maridhawa kuokoka na mizozo ya fedha, inashauri UM

UM umearifu ya kuwa fungu kubwa la mataifa yanayoendelea hivi sasa yanafanana na waathiriwa wasio hatia wa ile mizozo ya fedha iliopamba karibuni kwenye soko la kimataifa, wakati mataifa tajiri, yaliosababisha mzozo huo, hayajaonyesha dhamira ya kuzisaidia nchi maskini katu kukabiliana na mgogoro huu wa fedha.

Vifo vya watoto wachanga vimeteremeka karibuni, imeripoti WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) limewasilisha ripoti mpya ya maendeleo inayofungamana na zile juhudi za kuyatekeleza, kwa wakati, Malengo ya Maendeleo ya Milenia yanayohusu juhudi za kupunguza vifo vya watoto wachanga ulimwenguni.

Dozi bilioni 5 zaashiriwa kutayarishwa na makampuni ya madawa kupambana na homa ya H1N1

Dktr Margaret Chan, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameripoti ya kuwa hali ya kawaida ikijiri, kuna uwezekano kwa makampuni ya madawa ya kimataifa yakamudu kuharakisha utengenezaji wa dozi bilioni 4.9 za chanjo dhidi ya vimelea vya homa mpya ya mafua ya H1N1 katika kipindi cha mwaka mmoja.

UNFCCC imeripoti maendeleo kwenye majadiliano kuhusu udhibiti wa mabadiliko ya hali ya hewa duniani

Taasisi ya UM ya juu ya Utendaji wa Mkataba wa Kudhibiti Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani (UNFCCC) imetoa ripoti rasmi, ya kurasa 53, yenye mapendekezo kadha wa kadha, ya kuzingatiwa na kutekelezwa na mataifa yote wanachama, ikijumlisha mataifa tajiri na maskini, ili kudhibiti bora taathira haribifu zinazochochewa na hali ya hewa isio ya kikawaida wakati nchi wanachama zitakapokutana Copenhagen, baada ya siku 200 zijazo.