Asia Pasifiki

Siku ya Mazingira Duniani

Siku ya leo, tarehe 05 Juni (2009) huadhimishwa kila mwaka na UM kuwa ni \'Siku ya Mazingira Duniani\'. Lengo hasa la siku hii ni kuendeleza mwamko unaofaa, miongoni mwa umma wa kimataifa, kuhusu mazingira, kwa ujumla, na kufahamishana hatari inayokabili maumbile haya, na pia kuwahamasisha wanadamu kuwa mawakala wa kuwasilisha mabadiliko yatakayosaidia kuhifadhi mazingira na kudumisha maendeleo.

KM kupongeza risala ya Raisi wa Marekani kukuza uhusiano mwema na ulimwengu wa Waislam

KM Ban Ki-moon, kwa kupitia msemaji wake, ameripotiwa kuipongeza hotuba ya Raisi Barack Obama wa Marekani, alioiwakilisha kwenye Chuo Kikuu cha Cairo Alkhamisi ya leo, ambapo alizingatia uhusiano mpya baina ya Marekani na mataifa ya KiIslam. .

UN-HABITAT/UNIFEM yatashirikiana kupiga vita udhalilishaji na utumiaji mabavu dhidi ya wanawake

Mashirika mawili ya UM, yaani lile shirika juu ya makazi, UN-HABITAT, na lile shirika linalohusika na mfuko wa maendeleo kwa wanawake, UNIFEM, yameshirikiana rasmi kujumuika bia kukabiliana na tatizo la udhalilishaji na matumizi ya mabavu dhidi ya wanawake na watoto wa kike, katika miji ya mataifa yanayoendelea.

FAO inasema akiba ya chakula duniani imetulia mwaka huu

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limetoa ripoti yenye kuashiria mavuno ya nafaka, na akiba ya chakula kwa mwaka huu, hayatodhurika kiuchumi katika soko la kimataifa, kama ilivyotukia katika 2008, ambapo bei ya juu ya chakula ilisababisha mtafaruku na hali ya hatari kimataifa.

IFAD inayahimiza mataifa Afrika kukipa kilimo umuhimu kupambana na matatizo ya fedha

Kanayo F. Nwanze, Raisi wa Shirika la UM linalohusika na ukomeshaji wa ufukara na umaskini wa vijijini, yaani Shirika la Kimataifa juu ya Maendeleo na Kilimo (IFAD) ameshauri kwamba serikali za Afrika, zenye kutunza na kuhudumia kimaendeleo sekta ya kilimo, ndizo zitofanikiwa kudhibiti, kwa wastani, athari mbaya zinazoletwa na migogoro ya fedha duniani.

BK kupitisha azimio la kutiaka UM kuchunguza athari hatari ya mabadiliko ya hali ya hewa dhidi ya usalama

Ijumatanao, Baraza Kuu (BK) la UM, kwenye kikao cha wawakilishi wote lilipitisha, kwa kauli moja, azimio lenye kuyahimiza mashirika na taasisi zote za UM kufanya uchunguzi wa kuzingatia uwezekano wa kuzuka madhara haribifu dhidi ya usalama na amani duniani, kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, pindi jumuiya ya kimataifa itashindwa kuyadhibiti maafa hayo mapema.

Huduma za kilimo ni muhimu kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani: FAO

Juhudi za kufarajia maendeleo yanayosarifika kwenye sekta ya kilimo, hasa katika nchi zinazoendelea, ndio kadhia muhimu pekee yenye uwezo wa kudhibiti bora mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa duniani, na katika kupunguza njaa na ufukara, imeeleza Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO).

Takwimu mpya juu ya homa ya mafua ya A(H1N1)

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kuwa linazingatia kupandisha juu kipeo cha hadhari ya maambukizo ya homa ya mafua ya A(H1N1) ulimwenguni, kutoka daraja ya tano hadi daraja ya juu kabisa ya sita, kwa sababu ya kuendelea kwa maambukizo ya ugonjwa huu katika dunia.

Nchi zinazotunza vinasaba vya mimea anuwai kufadhiliwa msaada wa fedha na taasisi ya kimataifa

Mkutano wa Hadhi ya Juu wa wajumbe wa Bodi la Utawala la Taasisi ya Kutekeleza Mkataba wa Kimataifa Kutunza Rasilmali ya Vinasaba vya Mimea kwa Chakula na Kilimo, unaofanyika hivi sasa mjini Tunis, Tunisia umetangaza kuwa mataifa yanayoendelea 11 yanayotekeleza ile miradi ya kuhifadhi akiba ya mbegu za mimea kwa chakula na kutunza vinasaba vya mazao makuu, yatafadhiliwa msaada wa dola 500,000.

Mizozo ya ajira duniani inasailiwa na ILO kwenye mkutano wa mwaka Geneva

Shirika la UM juu y Haki za Wafanyakazi (ILO) litaanzisha Mkutano wa Mwaka mjini Geneva hapo kesho, tarehe 03 Juni, ambapo majadiliano yake yataendelea hadi Juni 19.