Kila sekunde 24 mtu mmoja anakufa kwenye ajali ya barabarani! Ndivyo ulivyoanza ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika maadhimisho ya leo ya siku ya kukumbuka waliopoteza maisha au kujeruhiwa kutokana na ajali za barabarani.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la kuhudumia watoto UNICEF, la mpango wa maendeleo UNDP na linaloshughulikia masuala ya wanawake UN Women leo yamezindua ripoti ya matokeo ya mkakati wa kukabiliana na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana ujulikanao kama “sportlight Initiative” kwa mwaka 2020 na 2021.
Watoto waliozaliwa baada ya mama zao kubakwa katika mazingira ya vita na mama zao kunyanyapaliwa, kutengwa, na kunyimwa rasilimali, wanakabiliwa na ubaguzi kwa njia nyingi na katika nyanja nyingi, pamoja na kutengwa na jamii zao wenyewe
Ufugaji wa kuhamahama, ni njia ya kitamaduni ya ufugaji, ambayo inawaajiri zaidi ya watu milioni 200 kwenye nchi 100 kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO.
Kura ya maoni iliyoendeshwa katika nchi 21 ikihusisha watoto na watu wazima imeonesha kuwa watoto wanaamini dunia inakuwa bora zaidi huku watu wazima wakiwa na shaka na shuku.
Kiwango cha utumaji fedha kwenda nchi za kipato cha chini na kati kinatarajiwa kuwa kimeongezeka kwa asilimia 7.3 na kufikia dola bilioni 589 mwaka huu wa 2021 tofauti na ilivyokadiriwa awali kutokana na hofu ya janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.
Leo ni siku ya kuchukua hatua kwa ajili ya kutokomeza saratani ya shingo ya uzazi. Kukiwa na wanawake zaidi ya 300,000 wanaokufa kila mwaka kutokana na saratani ya shingo ya uzazi shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linaungana na wadau kutoka kila pembe ya dunia kuadhimisha siku hii muhimu.
Kuzuia migogoro ndio nguzo kuu ya kuhakikisha amani ya kudumu duniani amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza kwenye mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama hii leo mjini New York Marekani uliojikita katika mada ya “amani na usalama kupitia njia za kidiplomasia za kuzuia migogoro.”
Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR inaonesha kuwa jamii ya kimataifa imeitikia vema wito wa kuwajibika pamoja katika kusaidia wakimbizi kupitia mkataba wa kimataifa wa wakimbizi, GCR.
Kwa wanufaika wa mpango wa mlo shuleni watafurahia sana kusikia taarifa hii iliyotolewa leo na mashirika matano ya Umoja wa Mataifa ya kuhakikisha kuwa kila mtoto anapata mlo bora shuleni ifikapo mwaka 2030.