Kuelekea kilele cha siku ya UKIMWI Duniani Desemba 1, Shirika la Umoja wa Mataifa la kufanikisha upatikanaji wa dawa za tiba kwa gharama nafuu, UNITAID limesema usumbufu na ucheleweshaji wa huduma za VVU unaosababishwa na janga la COVID-19 ulisababisha kupungua kwa vifaa vya upimaji na utambuzi wa VVU kwa kiwango kikubwa ambacho hakijawahi kuonekana ndani ya miongo miwili.