"Sasa ni wakati wa kuondoa silaha za nyuklia kutoka kwenye ulimwengu huu, na kuanzisha enzi mpya ya mazungumzo, uaminifu na amani", amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres Jumapili, katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya Kukomesha silaha za nyuklia.