Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema maadhimisho ya kimataifa ya siku ya kujindaa dhidi ya majanga yamekuja katika kipindi ambacho ni muafaka na kuakisi kile ambacho kinapaswa kufanywa ili kuepuka madhara makubwa.
Wakati wa janga la COVID-19 pengo la ukosefu wa usawa kati ya matajiri na maskini limeongezeka zaidi, halikadhalika umaskini, ikiwa ni mara ya kwanza katika miongo kadhaa. Katika sehemu hii ya pili ya mfululizo wa makala kuhusu jinsi COVID-19 imebadili dunia, tunaangazia jinsi janga hilo limerudisha nyuma juhudi za kujenga jamii zenye usawa zaidi.
Mwaka 2020 ukielekea ukingoni, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya idadi ya watu, UNFPA, Dkt. Natalia Kanem amesema mwaka huu wa 2020 ulikuwa ni mwaka wa janga kuu zaidi kwa wanawake na wasichana ambao tayari walikuwa kwenye masahibu hata kabla ya janga hilo.
Ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona au COVID-19 uko kila pahali na katika mwaka 2020 ulisambaa na kuleta madhara makubwa yaliyosababisha janga la dunia ambalo mapana yake hayakutarajiwa. Katika mfululizo wa makala sita juu ya mwaka huu wa mtikisiko, UN News inamulika athari za ugonjwa huu kwa watu kwenye maeneo mbalimbali ya dunia na suluhisho ambazo Umoja wa Mataifa umependekeza kufuatia janga hili. Katika makala hii ya kwanza tunamulika mambo ya msingi katika miezi 12 ya mwaka huu wa 2020.
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO limesema linashirikiana na wanasayansi ili kuelewa aina mpya ya virusi vya COVID-19 vilivyoripotiwa huko Afrika Kusini na Uingereza.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) limetimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwake ambapo Kamishna Mkuu wa shirika hilo Filippo Grandi amesema “niondoeni kwenye jukumu hili” kwa kushughulikia visababishi vya mamilioni ya watu kukimbia makwao kutokanana vita na ukosefu wa usalama.
Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP kupitia ripoti yake mpya limeonya kuwa nchi lazima zibuni njia zao za maendeleo ili kupunguza uharibifu wa mazingira na ulimwengu wa asili, la sivyo ni kuhatarisha maendeleo ya ubinadamu kwa ujumla.
Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP wiki hii limelifungua tena soko kubwa la wakulima kwenye kambi ya wakimbizi wa Rohingya ya Cox’s Bazar nchini Bangladesh baada ya kulifunga kwa miezi kadhaa kufuatia mlipuko wa janga la corona au COVID-19. Soko hilo ambalo ni sehemu ya mradi wa WFP ni neema sio tu kwa wakimbizi bali pia jamii inayowahifadhi.
Ujira wa wahamiaji ugenini kwa wastani ni chini ya asilimia 13 kulinganisha na wafanyakazi wenyeji katika nchi za kipato cha juu, imesema ripoti mpya ya shirika la kazi la Umoja wa Mataifa, ILO, iliyotolewa leo mjini Geneva, Uswisi.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia watoto duniani UNICEF la afya WHO leo yameonya kwamba ukosefu wa maji katika vituo vya huduma za afya unawaweka wafanyakazi na wagonjwa katika hatari kubwa ya maambukizi ya corona au COVID-19.