Umoja wa Mataifa leo umezindua mkakati wake mpya wa kuimarisha mchango wa takribani vijana bilioni 2 duniani kwa lengo kukuza amani, uadilifu pamoja na kuwa na dunia endelevu.
Umoja wa Mataifa leo umepitisha azimio la kumuenzi Nelson Mandela kutokana na mchango wake katika kusongesha utu, amani na haki za binadamu siyo tu nchini mwake bali duniani kote kwa ujumla. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.
Leo ni siku ya amani duniani ambapo Umoja wa Mataifa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo ametaka watu wasikate tamaa katika kusongesha amani licha ya vikwazo vilivyopo.
Umoja wa Mataifa leo utakuwa na tukio maalum la kumkumbuka Katibu wake mkuu wa 7 Kofi Annan aliyefariki dunia mwezi uliopita huko Uswisi na kuzikwa wiki iliyopita nyumbani kwake nchini Ghana.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema ingawa ushirikiano wa kimataifa unakumbwa na zahma, yeyé binafsi bado anaamini ndio njia sahihi ya kutatua matatizo yanayokumba dunia wakati huu wa utandawazi.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amekaribisha matokeo yaliyofikiwa kwenye mkutaon wa tatu wa mwaka kati ya viongozi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK na Jamhuri ya Korea ijulikanayo pia kama Korea Kusini.
Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO kuhusu hali ya chakula duniani inasema kuwa migogoro pamoja na mabadiliko ya tabianchi vinaendelea kuwa chanzo cha ukosefu wa uhakika wa chakula katika mataifa 39 duniani.
Benki ya Dunia imechukua hatua kusaidia Bangladesh kuimarisha huduma za afya ili nchi hiyo iweze kukabiliana na mahitaji ya wakimbizi wa Rohingya waliosaka hifadhi eneo la Cox’s Baz ar nchini humo.