Kuna haja ya kuunda ushirika mpya kati ya serikali, makundi ya kulinda wanyama na mazingira pamoja na jamii katika juhudi za kushughulikia ulinzi wa mazingira kama chanzo cha kujenga uchumi endelevu.
Kikosi kazi maalumu kimeundwa nchini Bangladeshi ili kuhakikisha usalama wa maelfu ya wakimbizi wa Myanmar na tendo ambao sasa wanaranda kwenye makazi ya wakimbizi hao.
Makwa 2017 kwa ujumla hakukuwa na mafanikio makubwa sana katika ulingo wa siasa kwa wanawake japo ushiriki wao katika masuala ya uchaguzi uliongezeka kiasi.
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya watetezi wa haki za binadamu inaonyesha kama watu hao wanaishi na vitisho dhidi yao na hivyo mataifa kushindwa kutekeleza wajibu wake kuhusu suala hili.
Ripoti ya Februari ya shirika la chakula na kilimo duniani FAO imebaini ongezeko la asilimia 1.1 la bei ya nafaka duniani Ikilinganishwa na mwezi Januari mwaka huu.
Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria Steffan de Mistura leo amesema Umoja wa Mataifa asilani hautokata tamaa Syria na utaendelea kusisitiza haja ya usitishaji mapigano kunusuru maisha ya watu.