Kampeni ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa kutanabaisha umuhimu wa chanjo katika kuokoa maisha hususani ya watoto itamalizika Jumapili wiki hii baada ya wiki nzima iliyoambatana na chanjo, mafunzo, maonesho na mijadala duniani kote.
Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT mwezi huu liliandaa mkutano wa kimataifa mjini Nairobi Kenya yaliko makao makuu ya shirika hilo na kuhudhuriwa na wakilishi kutoka nchi mbalimbali duniani.
Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linazinduia oparesheni ya dharura ya lishe na chakula ili kutoa huduma kwa watu milioni 3.5 wanaokabiliwa na njaa nchini Korea Kaskazini.
Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na madawa ya kulevya na uhalifu UNODC ametoa wito kwa sekta za umma na za kibinafsi kwenye nchi zilizostawi duniani kuchukua hatua ambazo zinaweza kuangamiza ufisadi akisema kuwa suala hilo linaweza kuzua mizozo.
Utafiti ulioendeshwa na Umoja wa Mataifa unaonyesha kuwa programu za elimu ya ujinsia kwa vijana zitakuwa za gharama ya chini ikiwa zitaunganishwa na kufanywa kuwa za lazima.
Umoja wa Mataifa kupitia kitengo chake cha upashaji habari, DPI kimeendelea kuongeza uwigo wa kutumia vyanzo mbalimbali ili kuhakikisha kwamba masuala muhimu yanayohusu umoja huo yanasambazwa kadri inavyotakiwa ulimwenguni kote.
Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia masuala ya kibinadamu kwa kuhakikisha msaada wa haraka kwa watu walioathirika na vita na majanga ya asili CERF, mwaka jana ulitenga dola milioni 415 ili kuyawezesha mashirika ya misaada kuwasaidia watu milioni 22 katika nchi 45.
Mwaka huu wa 2011 siku ya kimataifa ya usalama na afya kazini inajikita katika kutumia kama nyenzo mifumo ya utawala inayoshughulika na usalama na afya kazini ili kuendelea kuzuia matukio na ajali kazini.