Shirika la afya duani WHO, mfuko wa kimataifa wa kupambana na kifua kikuu, ukimwi na malaria na wadau wa kutokomeza kifua kikuu wametoa wito kwa viongozi wa dunia kuongeza juhudi za wajibu wao katika kufikia lengo la kuwapima na kuwatibu mamilioni ya watu wenye kifua kikuu kilichokuwa sugu dhidi ya madawa mchanganyiko (MDR-TB) kati ya mwaka huu 2011 na 2015.