Ripoti ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa biashara na maendeleo UNCTAD iliyotolewa leo inasema uzalishaji wa chuma cha pua ulipungua sana mwaka jana lakini mahitaji ya bidhaa hiyo yamehakikisha biashara inaendelea tena.
Masuala yanayohusu Kosovo na mkutano wa ngazi za juu wa upokonyaji silaha wa Septemba ndizo zimekuwa ajenda kuu leo kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Serbia Vuk Jeremic.
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP na mfuko wa The Nippon leo wamezindua rasmi mjini Nairobi shindalo la tuzo ya UNEP ya Sasakawa kwa mwaka 2011.
Zaidi ya wahudumu wa afua 20,000 wa kujitolea wanaendelea kuzuru nyumba hadi nyumba wakitoa chanjo kwa watoto dhidi ya polio nchini Afghanistan kama moja ya kampeni ya Umoja wa Mataifa ya kuwachanja watoto milioni 8 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Wadau wa misaada nchini Kyrgyzstan leo wametoa wito mpya wa dola milioni 96 kwa ajili ya kuwasaidia eneo la kusini mwa nchi hiyo kulikozuka machafuko mwezi Juni na kuathiri watu 400,000.