Asia Pasifiki

Vizazi vyote tuungane kuwasaidia vijana : Guterres

Ikiwa leo ni siku ya vijana duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa jamii kuwasaidia vijana kwa kuwekeza kwenye kuwapatia elimu na kuwajengea uwezo wa kiujuzi kupitia mikutano pamoja na kufanya mabadiliko katika mifumo ya elimu.

Cryptocurrency: UNCTAD yatangaza sera 3 zakufuatwa katika matumizi ya sarafu za kidijitali

Kamati ya  Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo UNCTAD imetoa mapendekezo ya sera tatu zinazoweza kutumiwa na nchi zinazoendelea kufuatia kuongezeka kwa matumizi ya sarafu za kidijitali au Cryptocurrency wakati huu ambapo nchi nyingi hazina sera wala mifumo madhubuti ya udhibiti na matumizi yake kwa jamii.

Teknolojia ya kuchuja maji kwenye mabwawa ya samaki yaongeza kiwango cha kamba 

Nchini Thailand, neema imerejea tena kwa wafugaji wa Kamba wadogo baada ya teknolojia mpya ya kuchuja maji na kulisha viumbe hao kusaidia kuondoa changamoto waliyopata awali ya milipuko ya magonjwa kutokana na uchafu wa maji kwenye mabwawa wanayofugia. 
 

Wiki ya unyonyeshaji: Usaidizi zaidi unahitajika kwa familia zilizopo katika mazingira hatarishi

Wiki ya Unyonyeshaji watoto maziwa ya mama duniani imeanza rasmi hii leo chini ya kauli mbiu yake isemayo Kuongeza Unyonyeshaji: Elimisha na Usaidizi, Umoja wa Mataifa unatoa wito kwa serikali kutenga rasilimali zaidi ili kulinda, kukuza, na kusaidia sera na programu za unyonyeshaji, haswa kwa familia zilizo hatarini zaidi ambazo zinaishi katika mazingira ya dharura.

Fahamu kuhusu Homa Kali ya Ini na hatua za kujikinga

Tarehe 28 mwezi Julai kila mwaka ni siku ya Homa ya Ini duniani na mwaka huu shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO linaangazia homa kali ya ini ambayo idadi ya wagonjwa inazidi kuongezeka na inaambukiza watoto. Kinachotia hofu ni kwamba hadi sasa aina hii ya homa ya ini chanzo chake hakijafahamika.

Dunia kushuhudia kudorora zaidi kwa uchumi: IMF

Ripoti ya hali ya uchumi kwa robo ya pili ya mwaka huu wa 2022 ambao ni mwezi Aprili hadi Juni ambayo imetolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF imesema matarajio ya ukuaji wa uchumi duniani yanazidi kukumbwa na kiza na yanakosa uhakika na kwamba matumaini ya uchumi kukwamuka mwaka 2021 yanazidi kuyoyoma mwaka huu wa 2022. 

Kuzama majini ni sababu kuu ya vifo vitokanavyo na ajali:WHO

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuzuia kuzama majini duniani Shirika la Umoja wa Afya duniani WHO limetoa wito kwa watu wote duniani kuongeza juhudi za kupunguza vifo vitokanavyo na watu kuzama kwenye maji, huku likitoa mapendekezo sita ya kusaidia kupunguza vifo na ajali zinazosababishwa na watu kuzama majini duniani kote. 

COVID-19 yarudisha nyuma utoaji chanjo kwa watoto kwa miongo mitatu

Licha ya mwaka 2021 kutegemewa utakuwa mwaka bora wa utoaji chanjo kwa watoto wachanga baada ya janga la COVID-19 kuvuruga utoaji chanjo mwaka 2019 na 2020, ripoti iliyotolewa leo na Umoja wa Mataifa imeonyesha kiwango cha utoaji chanjo duniani kimeendelea kupungua maradufu na kurudisha takwimu kwa miongo mitatu nyuma huku watoto milioni 25 wakikosa chanjo muhimu za kuokoa maisha yao.

WHO kuchunguza kuenea kwa homa kali ya ini isiyojulikana

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO limezindua utafiti duniani kote wenye lengo la kubaini idadi halisi na kiwango cha aina ya ugonjwa wa homa ya ini kali, Hepatitis miongoni mwa watoto, ambao ni tofauti na aina zote za homa ya ini zinazotambulika, wakati huu ambao ugonjwa huo umeripotiwa katika kanda 5 za WHO isipokuwa barani Afrika.

Sayansi na sera zishirikiane ili kusaidia bahari

Baada ya siku tano za mijadala na maonesho mbalimbali, mkutano wa pili kuhusu baharí umefikia tamati huko Lisbon nchini Ureno ambako Miguel de Serpa Soares ambaye ni Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kisheria amesema mwelekeo wa kulinda na kuhifadhi baharí unatia matumaini kwa kuzingatia yaliyokubaliwa, changamoto zilizoko sambamba na fursa.