Asia Pasifiki

Kamishna Mkuu juu ya wahamiaji azuru Pakistan kutathminia hali ya waathirika mapigano

António Guterres, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) Alkhamisi alianza ziara rasmi ya siku tatu katika Pakistan, kufanya tathmini ya mahitaji ya dharura ya kihali ya raia 800,000 waliong\'olewa makazi, kutokana na mapigano makali yalioshtadi karibuni baina ya vikosi vya Serikali na wapambanaji wapinzani, kwenye eneo la kaskazini-magharibi.

Baraza la Usalama lashtumu vikali kundi la LTTE Sri Lanka kwa "ugaidi ulioselelea"

Ijumatano Baraza la Usalama limearifu kuingiwa wahka mkuu juu ya kuongezeka kwa uharibifu wa hali ya kiutu katika Sri Lanka, kwa sababu ya mapigano makali katika Sri Lanka baina ya vikosi vya Serikali na kundi la wapinzani la LTTE.

Mikutano ziada kwenye Makao Makuu

Mikutano kadha mengine iliofanyika Ijumatano hapa Makao Makuu ni kama ifuatavyo: Kwenye Ukumbi wa Baraza la Udhamini, wajumbe wa kimataifa walikutana kuzingatia hatua za utendaji za dharura, kukomesha biashara haramu ya kutorosha watu makwao wanaotumiwa kwenye ajira za kulazimishwa.

Miradi ya kuimarisha miundombinu ya miji inazingatiwa na mameya

Ijumatano ya leo, kwenye Makao Makuu ya UM, wamekusanyika mameya na wawakilishi mbalimbali kutoka miji mikuu kadha ya ulimwengu, kuhudhuria Mkutano wa kuzingatia taratibu mpya za kuandaa miundombinu imara itakayotumiwa katika miji.

Ripoti ya 26 ya WHO juu ya Homa ya A(H1N1)

Wataalamu wa kimataifa wametoa taarifa inayohadharisha kwamba ikiwa walimwengu hawatofanikiwa kudhibiti bora maambukizi ya homa ya mafua ya virusi vya A(H1N1), yanayotendeka miongoni mwa wanadamu, inaashiriwa katika miezi sita hadi tisa ijayo, kuna hatari ya maradhi haya kupevuka na kuwakilisha "janga jipya hatari la afya ya jamii kimataifa".

Mashirika ya WFP/WHO yahudumia kihali raia waathirika wa mapigano Sri Lanka

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetoa ilani inayohadharisha kwamba pindi halitafadhiliwa msaada wa dharura wa dola milioni 40, kuhudumia chakula umma ulioathirika na mapigano katika Sri Lanka, litashindwa kununua chakula, kuanzia mwisho wa Julai ili kunusuru maisha ya wahamiaji.

Makundi yanayopigana Sri Lanka yatakiwa kuhishimu usalama wa raia

Verinoque Taveau, Msemaji wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) aliwaambia waandishi habari Geneva kwamba makundi yanayopambana katika Sri Lanka, yaani vikosi vya Serikali na waasi wa kundi la LTTE [Tamil Tiger], yamenasihiwa na UNICEF kufanya kila wawezalo kuwahakikishia raia ushoroba wa kupita, bila ya kushambuliwa kwenye mazingira ya uhasama.

Mamia elfu ya raia wa kaskazini-magharibi katika Pakistan wahajiri makazi baada kuzuka mapigano

UM umepokea taarifa zilizothibitisha kushtadi kwa mapigano baina ya majeshi ya serikali na wapinzani kwenye bonde la Swat, liliopo kwenye Jimbo la Mpakani Kaskazini-Magharibi katika Pakistan, yaani katika Jimbo NWFP.

Riporti ya WHO kuhusu maambukizi ya homa ya H1N1

Takwimu mpya za maambukizo ya homa ya mafua ya A(H1N1) ulimwenguni, zilizothibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) mnamo Ijumaa ya tarehe 08 Mei (2009) ni kama ifuatavyo: Jumla ya watu 2500 waliripotiwa rasmi kuambukizwa na homa ya mafua ya H1N1 katika mataifa 25, ikijumlisha Brazil, kwa mara ya kwanza tangu tatizo hili la afya kuzuka.

Haki ya kupata chakula ni haki msingi ya kiutu, asisitiza De Schutter

Olivier De Schutter, Mkariri Maalumu juu ya haki ya chakula ameiambia Kamisheni ya UM juu ya Maendeleo Yanayosarifika kwamba umma wa kimataifa unalazimika kuandaa, kidharura miradi madhubuti itakayoimarisha na kudumisha mifumo ya kuzalisha chakula kwa wingi, kwenye mazingira ya ulimwengu wa sasa, mazingira yaliokabiliwa na madhara kadha wa kadha yanayochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa na kupungua kwa maliasili duniani.