Umoja wa Mataifa na Kamati ya Tokyo ya maandalizi ya michezo ya olimpiki inayohusisha ile ya kawaida na ya watu wenye ulemavu wametiliana saini makubaliano yenye nia ya kusongesha mbele maendeleo endelevu, SDGs kupitia michezo itakayofanyika mjini Tokyo nchini Japan mwaka 2020.
Katika kuitikia changamoto za elimu miongoni mwa jamii ya wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladesh, dola milioni 12 zimetolewa kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa matatu ili kuhakikisha kwamba watoto wakimbizi na wenyeji 88,500 wamepata elimu.
Maadhimisho ya wiki ya kuhamasisha umma kuhusu matumizi ya viuavijasumu ikiendelea, Umoja wa Mataifa umesema wakulima wana dhima muhimu katika kupunguza usugu wa dawa hizo kwa kutumia mbinu bora za usafi katika shughuli zao za kila siku.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema sasa kuna matumaini makubwa ya kupitishwa kwa mkataba wa kimataifa kuhusu wakimbiz na wahamiaji, GCM mwezi ujao.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi , UNHCR linaunga mkono mchakato endelevu wa kuwarejesha nyumbani kwa hiyari wakimbizi wa Rohingya au watakapochagua endapo zoezi hilo lizingatia misngi ya haki za binadamu , usalama na utu na litashirikiana na wadau wote kutimiza azma hii.
Wakati dunia ikihaha kusaka mbinu za kukabiliana na uchafuzi wa mazingira, sekta ya ubunifu wa mitindo nayo imeshachukua hatua ili kuhakikisha bidhaa zake haziharibu mazingira.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema anatiwa hofu na hatua ya rais wa Sri Lanka ya kuvunja bunge la taifa hilo na kutangaza uchaguzi mpya hapo mwakani.
Kuelekea jukwaa la amani litakaloanza kesho huko Paris, Ufaransa, Rais wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD Gilbert F. Houngbo, amesema atatumia kusanyiko hilo kuwaeleza viongozi wa dunia juu ya umuhimu wa kuwekeza vijijini.
Pengine si wengi wanaoiingia katika mghahawa unaouza mathalani burger yaani nyama iliyofunikwa kwa mkate, wanaowaza kuwa chakula hicho wanachokinunua ni sawa na kushiriki katika kuharibu mazingira. Harakati za binadamu katika kutengeneza nyama ni njia mojawapo za uharibifu unaoacha alama duniani.
Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limetoa wito wa kuhakikisha chakula hakipotei au kutupwa hovyo ili kulinda virutubisho na lishe muhimu kwa ajili ya maisha ya binadamu.