Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na kampuni ya Mattel, Inc.,umezindua aina mpya ya mawasiliano ya kufikisha ujumbe wa malengo ya maendeleo endelevu , SDGs kwa watoto wa shule za Chekechea.
Mahakama kuu nchini India imetengua baadhi ya vifungu katika sheria za makossa ya jinai nchini humo hususan kifungu namba 377 kinachoharamisha kundi la watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja, LGBTI. Uamuzi huo umepongezwa na taasisi mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limetoa taarifa mpya kuhusu bei ya vyakula kwa mwezi Agosti na kusema bei kwa ujumla ilibaki palepale, haikuongezeka wala kupungua.
Hali ya kupuuza na kutoheshimu misingi ya kimataifa ya haki za binadamu kunatishia haki za afya ya uzazi na kujamihiana kwa wanawake mkiwemo wenye ulemavu.
Onyo hilo limetolewa leo mjini Geneva Uswisi na wataalam wa masuala ya haki za binadamu.