Bandari muhimu nchini Yemen ya Hodeidah ambayo imekuwa ikiandamwa na mashambulizi kutoka kwa vikosi vinavyounga mkono serikali kwa wiki kadha, sasa iko taabani na huenda shambulio linguine moja tu la anga likuka kuwa janga lisilozuilika, kwa mujibu wa mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu nchini humo, OCHA.