Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani kukamatwa kwa majaji wawili wa Mahakama Kuu nchini Maldives ikisema ni ukiukwaji wa utawala wa sheria na uhuru wa mahakama kufanya kazi katika misingi yake.
Tumepoteza jemadari wa haki za binadamu, hiyo ndio kauli aliyoitoa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres baada ya habari za kifo cha Asma Jahangir kutangazwa Pakistan hii leo alikotoka na duniani kote.
Uchangamfu wa mashindano ya olimpiki ni ishara muhimu ya amani katika dunia ya leo, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres huko PyeongChang nchini Korea Kusini kunakofanyika mashindano hayo ya majira ya baridi.
Shirika la muungano wa skauti duniani (WOSM) na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP leo wamedumisha ushirikiano wao kuhusu masuala ya mazingira kwa kutambua changamoto kubwa zinazoikabili dunia hivi sasa na umuhimu wa mchango wa vijana katika kujenga dunia endelevu kandoni mwa jukwaa la kimataifa la miji mjini Kuala Lumpur.
Juma hili maelfu ya watu na hususani wanamichezo wanakusanyika mjini PyeongChang huko Jamhuri ya Korea, kwa ni ya kushiriki mashindano ya Olimpiki ambayo ni ya kirafiki, yenye mshikamano, na ya kuheshimiana.
Baada ya kuonekana kuwa wananufaika na walengwa kwa muda mrefu, wanawake sasa ni vinara wa kuleta mabadiliko katika miji endelevu, na hii imewezekana baada ya wenyewe kuwa mstari wa mbele kutambua shida zinazowakabili na majibu sahihi ya matatizo yao.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limeonya kwamba msimu wa pepo kali na mvua za monsoon utawaweka hatarini maelfu ya wakimbizi wa Rohingya walioko Bangladesh na hivyo likishirikiana na wadau wengine wanajiandaa kukabiliana na athari zake.