Wafanyakazi takriban wanane wa Umoja wa Mataifa wameuawa nchini Afghanistan hii leo na wengine kujeruhiwa baada ya waandamanaji kushambulia ofisi za Umoja wa Mataifa katika mji wa Mazar-i-Sharif Kaskazini mwa nchi hiyo.
Nusu ya mataifa 48 maskini zaidi duniani yanaweza kujikwamua kutoka kwa hali yaliyo sasa kwa muda wa maika kumi ikiwa yatafaidika na misaada ya kimaendeleo, kuondolewa kwa ushuru wa bidhaa yanayouza na pia kwa kuongeza maradufu mazao ya kilimo.
Mionzi hivi sasa inasafiri kutoka katika kinu cha nyuklia cha Japan kilichoharibiwa na tetemeko na tsunami kwenda katika nchi zingine, lakini shirika la afya duniani WHO linasema mionzi hiyo ya nje sio tishio.
Waakilishi wa serikali , viwanda vikubwa na watafiti wa mambo ya bahari wameungana kutafuta mbinu mpya za kukabiliana na tatizo la kuendelea kuchafuliwa kwa bahari kuu duniani.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa biashara ya utumwa ilisababisha mateso makubwa kwa mamilioni ya watu wasio na hatia kwa muda wa karne nne.
Serikali ya Libya haijaacha mashambulizi au kutangaza kusitisha mapigano kama ilivyotakiwa na azimio la baraza la usalama kwa mujibu wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.
Mcheza filamu mashuhuri na mjumbe maalumu wa amani wa Umoja wa Mataifa Michael Douglas amesema dunia inahitaji kuendelea kuisaidia Japan hasa wakati huu.
Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP kwa ushirikiano na mashirika yanayoandaa mashindano ya olimpiki ya mwaka 2014 yatakayoandaliwa mjini Sochi nchini Urusi wamejitolea kurekebisha uharibifu kwenye bonde la mto mmoja mihimu nchini humo.