Asia Pasifiki

Ban amesikitishwa na matumizi ya watoto kujitoa muhanga Pakistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesikitishwa na ripoti kwamba mtoto ametumiwa kufanya shambulio la leo la kujitoa muhanga kwenye kituo cha mafunzo ya kijeshi cha Mardan Kaskazini Magharibi mwa Pakistan.

Ujumbe maalumu wa UNESCO kuzuru Cambodia na Thailand

Ujumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa umetumwa kwenda Cambodia na Thailand ili kusaidia kutatua mzozo dhidi ya hekalu la Preah Vihear.

UM kutathmini madeni ya nje na haki za binadamu visiwa vya Solomon:

Mtaalamu binafsi wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu athari za madeni ya nje katika utekelezaji wa haki za binadamu Cephas Lumina atazuru visiwa vya Solomon kuanzia Jumatatu Ijayo Februari 14 hadi 18 kutathimini athari za mzigo wa madeni ya nje kwa nchi hiyo.

Tume za UM ni nguzo ya kuleta maendeleo:Migiro

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro amesisitiza kuwa tume za kimaeneo za Umoja wa Mataifa ndiyo nguzo katika juhudi za Umoja wa Mataifa za kupunguza umaskini na kunua maisha ya watu.

Wataalamu vijana kusaidia kuzipa pengo la upungufu wa maarifa

Kundi la wataalamu wa mawasiliano ya kopyuta limeunganisha nguvu ili kuzisaidia nchi zinazoendelea ambazo zinakabiliw a na changamoto ya kufikia malengo ya maendeleo mellenia kutokana na kuendelea kubaki nyuma kwenye maarifa ya kisayansi.

Bank ya Dunia yaonya kuhusu matatizo ya afya Asia:

Ripoti iliyotolewa leo na Bank ya dunia inaonya kwamba nchi za Asia Kusini zinakabiliwa na matatizo makubwa ya kiafya kukiwa na ongezeko la magonjwa kama ya kisukari, mfuta mwilini kupita kiasi na magonjwa mengine yasiyo ya kuambukiza.

UNICEF yawasaidia Wapakistani wanaokabiliwa na baridi:

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linakimbiza misaada muhimu kwa kwa njia ya helkopta kwa maelfu ya Wapakistan walionusurika na mafuriko ambao sasa wako katika hatari kutokana na msimu wa baridi kali.

Kodi ziondolewe katika madawa na vyandarua vya mbu:M-TAP

Mkutano maalumu wa kutathimini hali ya kupambana na malaria duniani umetoa wito wa kuondoa kodi katika madawa ya malaria, vyandarua vya mbu na bidhaa zingine za kuokoa maisha zinazohusiana na kukabili malaria.

WFP inaongeza msaada Sri Lanka baada ya athiri za mafuriko

Kwa mara ya pili katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja mvua kubwa za monsoon zimewalazimisha maelfu ya watu kuzikimbia nyumba zao nchini Sri Lanka baada ya kusababisha mafuriko katika maeneo mengi ya nchi hiyo.

Hatua zikichukuliwa kupunguza majanga maisha yatanusurika:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akizungumza kwenye mkutano huo wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa amesema mwaka jana ulighubikwa na majanga.