Asia Pasifiki

Washinda tuzo la Sasakawa

Miradi miwili iliyokuwa na shabaya ya kuhifadhi mazingira na kukaribisha maendeleo endelevu katika maeneo ya vijijini huko Latin Amerika na Asia imefaulu kushinda tuzo la UNEP ijulikanayo Sasakawa.

UNESCO yasema lugha mama ziko hatarini kupotea

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi na utamaduni UNESCO limeonyesha wasiwasi wake kuhusiana na kuanguka kwa lugha zinazotambulika kama lugha mama, kutokana na kukua kwa mfumo mpya unakumbatia lugha mtawanyiko.

Kuwekeza kwenye mapinduzi ya uchumi wa kijani ndiyo hatua muafaka-UM

Umoja wa Mataifa katika ripoti yake iliyozinduliwa leo imetilia muhimu juu ya uwekezaji kwenye maeneo muhimu kadhaa ambayo imesema kuwa yanaweza kuleta mabadiliko makubwa na kuibua uchumi wa kijani.

Hali ya hatari yatangazwa New Zealand-OCHA

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA imesema kumetolewa hali ya tahadhari katika eneo la kanisa huko New Zealand kufuatia tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha richter 6.3

Kikao cha Kamisheni juu ya hali ya wanawake chaanza New York

Kikao cha Kamisheni juu ya hali ya wanawake kimeanza leo mjini New York.

Wawakilishi wa serikali pamoja na makundi ya kiharakati zaidi ya 1,500 wanaweka zingatia lao kwenye majadiliano kuhusu nafasi ya mwanamke na mtoto wa kike kushiriki kwenye elimu, mafunzo na maeneo ya sayansi.

Kansa yaleta mzigo mpya kwa nchi maskini-WHO, IAEA

Mashirika ya Umoja wa mataifa yameonya kuwa ugonjwa wa kansa ambao kwa kiwango kikubwa ulisambaa zaidi katika nchi zilizoendelea sasa umepindukia na kuweka mzigo mpya kwa nchi maskini.

Mkutano wa kujadilia fursa za afya wafanyika Geneva

Kongamano la kujadilia njia bora zitazowawezesha watumiaji wa huduma za afya namna wanavyofikia kirahisi na huduma hizo, umeanza leo huko Geneva, kwa mkurugenzi wa shirika la afya duniani WHO kutoa wito kwa mataifa kubadilisha mwenendo wa kushughulia matatizo ya sekta ya afya.

Kuna maendeleo kwenye kufikia ustawi wa kijamii-ILO

Kuna hatua kubwa iliyopigwa kwa mataifa mbalimbali juu ya kuteleza mikakati ya kuboresha ustawi wa haki za kijamii.

Uchafuzi wa kimazingira kutokana na kemikali kusababisha athari kubwa

Kiwango kikubwa cha kemikali ya fosforas kinachotumiwa kama mbolea muhimu na kinachohitajika sana katika ukuaji wa binadamu kimekuwa kinapotea na kumwagwa mabarini kutokana na ufundi mdogo katika kilimo na kukosa kuejiuza maji machafu kama mbolea.

Shughuli za ulinzi wa amani zinataka ushirikiano zaidi- Alain Le Roy

Mashirikiano ya dhati baina ya Umoja wa Mataifa na washirika wake ndiyo nguzo muhimu inayoweza kufanikisha shabaya ya kuwepo kwa shughuli za vikosi vya uletaji amani.