Asia Pasifiki

Kuna sababu mpya zinazochangia wimbi la wakimbizi:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kuna ongezeko la wakimbizi kuzikimbia nchi zao kwa sababu tofauti na zile za vita na kukabiliwa na vifo.

Thamani ya uzalishaji wa opium Kusini Mashariki mwa Asia yaongezeka

Thamani ya uzalishaji wa mihadarati aiana ya opium Kusini Mashariki mwa Asia imeongezeka na kufikia dola milioni 219 kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC.

Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari kujikita katika habari na karne ya 21

Vyombo vya habari karne ya 21, mtazamo mpya na mipaka mipya hiyo ndio itakuwa kauli mbiu ya maadhimisho yajayo ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari hapo Mai 3 mwaka 2011.

Mwakilishi Maalumu wa Masuala ya chakula wa UM kuzuru Uchina kwa mara ya kwanza

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa wa haki ya chakula Olivier de Schuter atafanya ziara maalumu katika Jamhuri ya watu wa Uchina kuanzia Jumatano wiki hii hadi tarehe 23 Desemba 2010.

Magenge ya usafirishaji haramu wa watu yadhibitiwe:Ban

Vitendo vya usafirishaji haramu wa binadamu vimeendelea kuwafadisha magenge machache ya watu huku wanawake na watoto wakiendelea kuwa wahanga wakubwa wa matukio hayo.

Wataalamu wa Haki za Binadamu wa UM wahofia kusumbuliwa kwa watetezi wa haki Uchina

Wataalamu watatu wa haki za binadamu wameelezea hofu yao dhidi ya kusumbuliwa na kukamatwa kwa watetezi wa haki za binadamu nchini Uchina tangu kutangazwa kupewa tuzo ya Nobel kwa mpigania haki Liu Xiaobo miezi miwili iliyopita.

Wakimbizi Nepal waendelea kupata makao mapya:UNHCR

Mpango wa kuwapa makao maelfu wakimbizi kutoka Nepal uliozinduliwa miaka mitatu iliyopita umeshuhudia kupatikana kwa makao kwa zaidi ya idadi wa wakimbizi iliyowekwa ya wakimbizi 40,000.

Mafanikio makubwa yamepatikana kwenye mkutano uliomalizika Cancun:UM

Hatua mbalimbali zenye lengo la kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa zimeafikiwa kwenye mkutano wa kimataifa uliomalizika mwishoni mwa wiki mjini Cancun Mexico.

Ban aweka msukumo kwenye kampeni ya usafiri salama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameipa nguvu kampeni ya kuwa na usafiri salama barabarani na kuhimiza namna inavyowezekana kuwa na usafiri imara na salama.

Mkataba ya kibiashara kati ya India na Jumuiya ya Ulaya kuathiri upatikanaji wa madawa:UM

Mjumbe maluum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na afya nzuri Anand Grover amesema ameonya kuwa makubalino ya kibiashara kati ya India na Jumuiya ya ulaya huenda ikazuia mamilioni ya watu kupata madawa yanayookoa au kurefusha maisha.