Umoja wa Mataifa umetumia mchezo wa soka ili kuwafikia wahanga wa majanga ya kimaumbile yaliyotokea katika nchi za Haiti na Pakistan ambako mamia ya watu waliathiriwqa vibaya.
Nchi zinazoendelea zinapoteza kati ya dola bilioni 20 na bilioni 40 kila mwaka kwa sababu ya hogo, ubadhilifu na vitendo vingine vya kifisadi umesema muongozo mpya uliotolewa na Bank ya dunia.
Mataifa 59 ambayo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa yamehaidi kutoa kiasi cha dola milioni 358 kwa ajili kutunisha mfuko wa dharura unaotumika kukabili majanga CERF.
Muda wa majaji wanaohudumu kwenye mahakama za Umoja wa Mataifa za uhalifu dhidi ya vita vya Balkans vya miaka ya 1990 na mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 wameongezewa muda.
Wataalamu wa afya wanaotoa huduma za matibabu ya dharura nchini Pakistan nchi ambayo ilikubwa na mafuriko yaliyoharibu kabisa mifumo yote ya afya, wataendelea kubaki nchini humo hadi hapo May 2011.
Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF ni muhimu sana na ni chombo kinachoongoza duniani kutoa msaada wakati wa majanga amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.
Ili kuzuia na kutibu athari za ulevi wa kupindukia na matumizi ya mihadarati, shirika la afya duniani WHO leo limezindua ripoti ya kwanza ya dunia kuhusu nyezo zinazotumiwa hivi sasa kukabiliana na hofu ya matatizo hayo ya kiafya.