Asia Pasifiki

Mkataba kufuatilia kupotea kwa watu waanza kutekelezwa leo: UM

Mkataba muhimu wa kufuatilia kupotea kiholela au kwa lazima kwa watu unaanza kutekelezwa leo huku wataalamu wa Umoja wa Mataifa wenye jukumu la kuzisaidia familia kujua hatma ya wapi waliko jamaa zao waliopotea, wameyataka mataifa yote kuhakikisha wanakomesha uhalifu huo kwa kuwafikisha wahusika kwenye vyombo vya sheria.

Uchina yapiga hatua kutoka usalama wa chakula kuingia haki ya chakula: UM

Uchina imepiga hatua kubwa za kiuchumi na kijamii katika miongo mitatu iliyopita na kuwatoa mamilioni ya watu wake katika umasikini, kuwafaidisha na usalama wa chakula kutokana na mafanikio hayo.

Mkutano kuhusu mkataba wa Hali ya Hewa umemalizika Geneva

Mkutano wa kimataifa kuhusu mkataba wa hewa umemalizika mjini Geneva kwa mafanikio makubwa.

Waandishi habari wanaofanya kazi kwenye maeneo ya vita walindwe: UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO ambalo pia linapigania uhuru wa habari na wa kujieleza leo limetoa wito wa kuimarisha usalama kwa waandishi na wafanyakazi wengine wa sekta ya habari wanaofanya kazi kwenye maeneo ya vita au machafuko ya kijamii.

Baraza la Haki za Binadamu kukutana kujadili hali ya Ivory Coast

Wakati huohuo baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kesho Alhamisi Desemba 23 itafanya kikao maalumu kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Ivory Coast tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu Novemba 28.

Vijana waongoza ajenda kwenye mkutano wa baraza la usalama la UM

Vijana kutoka kote duniani wameelezea mtazamo wao kuhusu masuala wanayoayona kuwa muhimu kwenye mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York leo.

Bangladesh na IOM kukabiliana na usafirishaji haramu wa watu

Bangladesh mbioni kuanzisha sheria ya kukabiliana na biashara ya usafirishaji haramu wa binadamu

Bangladesh imeanzisha kipengele cha awali cha sheria yenye lengo la kukabiliana na biashara haramu ya usafirishaji binadamu.

Mwaka wa Bayo-Anuai umemalizika kwa mafanikio na kuundwa chombo kipya: UNEP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP linasema chombo kipya cha kimataifa chenye lengo la kukabiliana na kupotea kwa bayo-anuai, misitu muhimu kiuchumi duniani, viumbe vingine vya majini kimezaliwa jana, baada ya muafaka wa serikali na mkutano wa 65 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Serikali ya Indonesia, Viongozi wa Dini na UNICEF kuchagiza unyonyeshaji

Wakati serikali ya Indonesia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya kina mama wiki hii, viongozi wa serikali, viongozi wa dini kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wameungana kuchagiza umuhimu wa kunyonyesha watoto.

Mataifa lazima yatekeleze makubaliano ya Cancun:Figueres

Mkuu wa masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa leo ametoa wito kwa nchi kuchukua hatua kufuatia makubalino ya karibuni ya mkutano wa Cancun ya kukata kwa kiasi kikubwa gesi chafu na kuzindua taasisi mpya na fedha.