Wazungumzaji katika mkutano wa siku mbili wa wataalamu unaojadili changamoto za maendeleo zinazozikabili nchi masikini, wamesema mtazamo mpya ni lazima kama nchi masikini kabisa duniani ambazo hivi karibuni zimekumbwa na matatizo ya chakula na nishati, mtikisiko wa kiuchumi, na katika maeneo mengine majanga ya kiasili, zitataka kuepukana na matatizo haya.