Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limemtangaza mshindi wa mwaka huu wa tuzo ya wakimbizi iitwayo Nansen Refugee Award kuwa ni mwandishi mpiga picha wa Kiingereza Alixandra Fazzina.
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limealaani kuzamishwa kwa meli ya Jamhuri ya Korea hivi karibuni huku likisisitiza haja ya kuzuia mashambulio zaidi dhidi ya taifa hilo la Asia mashariki na ukanda mzima.
Watu zaidi ya miasita wamekutana msikitini karibu na mji wa Jalalabad Kusini mwa Kyrgystan katika juhudi za kupata maridhiano baiana ya jamii za Wauzbek na Wakyrgy.
Ripoti ya shirika la fedha duniani IMF katika nusu ya kwanza ya mwaka huu 2010 inaashiria kiwango cha ukuaji wa uchumi kitaongezeka na kufikia asilimia nne na nusu.