Baraza kuu la Umoja wa Mataifa leo limefanya kikao kisicho rasmi kuienzi kwa mara ya kwanza siku ya kimataifa ya Nelson Mandela ambayo itakuwa Jumapili Julai 18.
Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa lenye jukumu la kutetea uhuru wa vyombo vya habari leo ameelezea hofu yake juu ya kifo cha mwandishi wa habari wa India Hem Chandra Pandey.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesisitiza haja ya kuchagiza usalama wa watu kwa kuzingatia kwamba changamoto zinazoikabili dunia hivi sasa zinatishia maisha ya mamilioni na kurudisha nyuma juhudi za maendeleo.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wake wanakabiliwa na upungufu wa dola bilioni tano mwaka huu za kuweza kukabiliana na matatizo ya kibinadamu yanayoikumba dunia.
Australia, Indonesia na mfuko wa kimataifa Global Fund wamesaini makubaliano muhimu ambayo yataongeza msaada wa mipango ya kupambana na kifua kikuu nchini Indonesia.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kuratibu masuala ya misaada ya kibinadamu John Holmes ameliambia baraza la uchumi na jamii linalokutana mjini New York kuwa tunahitaji kutambua wapi ambako misaada ya kibinadamu ni lazima ipelekwe.
Mfuko wa kimataifa yaani Global Fund na makampuni yanayotengeneza dawa za malaria zenye ubora wamekamilisha makubaliano ya kupunguza bei ya dawa za malaria ili mamilioni wanaozihitaji waweze kumudu hususani watoto.