Mchezaji hodari wa kandanda wa timu ya Brazil ambaye pia ni balozi mwema wa shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP, Kaka, amewaomba mashabiki watakao tanzama Kombe la dunia litakalo fanyika mwaka huu nchini Afrika Kusini kuchangia katika juhudi za kupunguza tatizo la chakula.