Asia Pasifiki

UM: zaidi ya ajali asili 3 800 zilitokea muongo ulopita

Idara ya Umoja wa Mataifa ya kujaribu kupunguza maafa imeeleza kwamba mnamo muongo uliyopita kumekuwepo na ajali asili 3 800 zilizosababisha vifo vya watu 780 000. Idara hiyo inakadiria ajali asili hizo zimesababisha uharibifu wa mali wa kiasi cha dola bilioni 960.

UM unaondowa vikwazo dhidi ya maafisa 5 wa zamani wa Taliban

Maafisa watano wa zamani wa serekali ya Taliban wameondolewa kutoka orodha ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa kabla ya kuanza kwa mkutano muhimu wa kimataifa siku ya Alhamisi mjini London, unaotarajia kuzingatia juu ya mpango wa serekali ya Afghanistan kuwarai wanaharakati kubadilisha upande.

Viwango vya ukosefu kazi duniani vimefikia vya juu kabisa kuwahi kutokea

Idadi ya watu wanaopoteza ajira kote duniani imeongezeka kufikia viwango vya juu kabisa kuwahi kutokea katika historia, kukiwepo na karibu watu milioni 212 mwaka jana ambao hawakua na ajira.

Kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa mataifa yanayoendelea

Mkuu wa Idara ya kimataifa ya UM kwa ajili ya maendeleo ya kilimo, IFAD, anasema kilimo ndiyo inasukuma mbele ukuwaji wa uchumi wa mataifa yanoendelea kabla ya kuanza kwa mkutano wa wiki moja wa jopo la uchumi duniani huko Davos Uswisi.

UNCTAD: Uwekezaji wa Kigeni washuka sana mwaka 2009

Ripoti mpya ya Idara ya Biashara na maendeleo ya UM UNCTAD imegundua kwamba uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni FDI mwaka jana ulipungua katika kanda zote za dunia. Inaeleza kwamba mataifa yaliyoendelea yalishuhudia kuporomoka zaidi kwa uwekezaji mwaka 2008 na kuendelea kupunguka kwa mwaka 2009 kwa asili mia 41 zaidi.

UM unataraji uchumi dunia kufufua kidogo

Katika ripoti yake kuhusiana na hali ya uchumi duniani na matarajiyo yake UM umeeleza kwamba kuanzia robo ya pili ya mwaka jana, hali ya uchumi duniani imekua ikianza kurudi kua ya kawaida.

Lazima UM kuendelea na jukumu la mazungumzo ya hali ya hewa

Mkurugenzi mkuu wa Idara ya mazingira ya UM Achim Steiner anasema ni lazima kwa majadiliano ya kimataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani yabaki chini ya uwongozi wa UM hata ikiwa mkutano wa viongozi wa Copenhagen mwezi Disemba haukufanikiwa kuleta ufumbuzi.

Jumuia za kikanda lazima yachukuwe jukumu kubwa pamoja na UM kutanzua mizozo

Baraza la usalama lilijadili Alhamisi njia mbali mbali za kuimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa mataifa na jumuia za kikanda ili kukabiliana na mizozo ya dunia.

Maelfu na maelfu ya wakimbizi kupata mikopo

Maelfu na maelfu ya watu walopoteza makazi yao kote duniani watapata mikopo midogo ili kuweza kuanzisha biashara zao wenyewe na kuweza kujitegemea, kufuatia makubaliano kati ya Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji UNHCR na shirika la kutoa mikopo midogo iliyoanzishwa na mshindi wa tunzo ya Nobel Muhammad Yunus kutoka Bengladesh Grameen Trust.

UM unaihimiza Italia kupunguza chuki dhidi ya wageni

Wataalamu wawili wa haki za binadamu wa UM wanaohusika na wahamiaji na ubaguzi wamewahimiza wakuu wa Italia kuchukua hatua zinazohitajika kupunguza hali ya kuongezeka kwa chuki dhidi ya wafanyakazi wa kigeni.