Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa yupo ziarani nchini Mongolia ambapo hapo jana alieleza mshikamano wa Umoja wa Mataifa na nchi hiyo kuwa ni ishara ya amani katika ulimwengu wenye matatizo
Kamati ya Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo UNCTAD imetoa mapendekezo ya sera tatu zinazoweza kutumiwa na nchi zinazoendelea kufuatia kuongezeka kwa matumizi ya sarafu za kidijitali au Cryptocurrency wakati huu ambapo nchi nyingi hazina sera wala mifumo madhubuti ya udhibiti na matumizi yake kwa jamii.
Huku kukiwa na joto kali, ukame na moto wa nyika, sehemu nyingi za dunia zilikuwa zimepitia mojawapo ya Julai tatu zenye joto zaidi katika rekodi, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa WMO hii leo.
Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA, limetoa ombi la dola milioni 10.7 kwa ajili ya kutoa usaidizi wa kuokoa maisha kwa wanawake na wasichana zaidi ya milioni mbili nchini Sri Lanka.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anaendelea na ziara yake nchini Japan baada ya mapema hii leo Jumamosi kuhudhuria sherehe za kuadhimisha miaka 77 ya shambulio la mbomu la nyuklia la Hiroshima lilosababisha maafa ambayo athari zake zinaendelea kuonekana mpaka hii leo.
Ni jambo lisilokubalika kabisa kwa mataifa yenye silaha za nyuklia kukiri uwezekano wa vita vya nyuklia, Amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Maataifa Antonio Guterres, Jumamosi nchini Japan katika sherehe za kuadhimisha miaka 77 ya shambulio la bomu la nyuklia la Hiroshima.
Nchini Thailand, neema imerejea tena kwa wafugaji wa Kamba wadogo baada ya teknolojia mpya ya kuchuja maji na kulisha viumbe hao kusaidia kuondoa changamoto waliyopata awali ya milipuko ya magonjwa kutokana na uchafu wa maji kwenye mabwawa wanayofugia.
Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA, leo limetaja washindi 10 wa pamoja wa shindano la miradi bunifu inayoweza kuleta mabadiliko chanya na kuwezesha wanawake na wasichana duniani.
Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, limesema nchi zinapaswa kushirikiana kukomesha haraka kuenea kwa ugonjwa wa ndui ya nyani, au Monkeypox bila kujali utaifa, rangi ya mtu au dini, amesema afisa mwandamizi wa shirika hilo hii leo.
Wakati zaidi ya robo tatu ya watu wazima wote wanaoishi na Virusi vya UKIMWI VVU wanapata aina fulani ya matibabu, idadi ya watoto wanaofanya hivyo, inafikia asilimia 52 pekee.