Idadi ya watu wenye njaa duniani iliongezeka mwaka jana na kufikia watu milioni 828 ikiwa ni ongezeko la watu milioni 46 zaidi kutoka mwaka uliotanguliwa wa 2020, na milioni 150 tangu kuzuka kwa COVID-19, imesema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo ikiwa ni ushahidi tosha kuwa dunia inaenda mrama kutoka lengo lake la kutokomeza njaa, ukosefu wa uhakika wa chakula na utapiamlo wa aina zote ifikapo mwaka 2030.