Asia Pasifiki

Hakikisheni afya ya akili kwa watu wote si ndoto:Guterres

Janga la COVID-19 limekuwa na athari kubwa kwa afya ya akili ulimwenguni kote, na lazima hatua zichukuliwe ili "kukomesha ukosefu wa usawa uliofichuliwa na janga hilo", pamoja na upatikanaji wa huduma muhimu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya akili, inayoadhimishwa leo Jumapili Oktoba 10.

Posta ina mchango mkubwa kwa jamii na uchumi wetu:UN

Leo ni siku ya posta duniani na katika siku hii tunatambua mchango mkubwa na muhimu wa wahudumu wa posta kwa jamii zetu na uchumi wetu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Katika siku ya ndege kuhama ,Imba, ruka na paa kama ndege ili kuwalinda :UN

Leo ni siku ya ndege wanaohama duniani kaulimbiu mwaka huu ikiwa “Imba, ruka nap aa kama ndege” ambapo watu wote duniani wanaisherehekea kwa kampeni kubwa ya kimataifa yenye lengo la kuelimisha kuhusu Ndege wanaohama na haja ya ushirikiano wa kimataifa kuwalinda.

WHO imeeleza maana ya hali ya baada ya COVID-19 na msaada wa tiba

Ufafanuzi rasmi wa kwanza wa kitabibu wa kuishi na maradhi ya baada ya ugonjwa wa COVID", umekubaliwa kufuatia mashauriano ya kimataifa na kutolewa leo ili kusaidia kuongeza matibabu kwa wagonjwa, limesema shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO.

Mkakati wa kusambaza chanjo za COVID-19 duniani wazinduliwa 

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO leo limezindua Mkakati wa Kufikisha chanjo ya COVID-19  kwa asilimia 70 ya wakazi wa dunia ifikapo katikati ya mwaka ujao wa 2022 lengo likiwa ni kumaliza kile kilichoitwa mwenendo usio sahihi wa utoaji chanjo hizo katika mataifa maskini na yale tajiri na hivyo kuhakikisha kila mtu amekingwa dhidi ya ugonjwa huo. 

Umaskini umekithiri miongoni mwa makabila na makundi fulani duniani

Watu bilioni 1.3 katika nchi 109 duniani ni maskini wa kila hali na kiwango cha umaskini huo kinatofautiana kikabila, kwa kundi au rangi, hiyo ni kwa mujibu wa uchambuzi mpya kuhusu kiwango cha umaskini wa kila hali duniani ikiwemo kiafya, kielimu na kiwango cha maisha, uliotolewa leo na Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. 

Utapiamlo kwa watoto umefurutu ada Afghanistan:UNICEF/WFP 

Hali ya kutokuwa na uhakika wa chakula na vita nchini Afghanistan vimeongeza mara dufu tatizo la utapiamlo kwa watoto na kuzusha wasiwasi mkubwa kwa hatama ya watoto hao na familia zao yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na la mpango wa chakula duniani WFP ambayo sasa yametoa wito wa mshikamano kunusurua taifa hilo.

Changamoto za maji zinaongezeka duniani:WMO Ripoti

Usimamizi bora wa maji ni muhimu, pamoja na ufuatiliaji na tahadhari ya mapema, vingesaidia kupunguza shida zinazosababishwa na wingi auuhaba wa bidhaa hiyo adimu, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO.

COVID-19 inaacha kovu la kudumu katika afya ya akili ya watoto na vijana

Watoto na vijana watasalia na madhara ya ugonjwa wa Corona au COVID-19 kwa afya zao za akili na kimwili kwa miaka mingi ijayo, imesema ripoti mpya ya hali ya watoto duniani  SOWC ilyotolewa leo jijini New York, Marekani na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto ulimwenguni, UNICEF. 

COVID-19, mabadiliko ya tabianchi ni mwiba wa maendeleo mijini- UN

Katika maadhimisho siku ya makazi duniani, ambayo mwaka huu ina kaulimbiu "Kuongeza kasi ya hatua mijini ili kuwa na dunia isio na hewa ukaa", Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka kufanya kazi pamoja "ili kutumia uwezo wa mabadiliko kwa ajili ya hatua endelevu mijini".