Asia Pasifiki

Tusisahau kuwasaidia Waafghanistan na jamii zinazowapa hifadhi: UNHCR

“Sasa kupita wakati mwingine wowote tunahitaji kusimama na Waafghanistan ambao wamebeba gharama ya mizozo, kuwahakikishia kuwa hawajasahaulika”

UN yatoa wito wa ushirikiano wa kimataifa kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kufikia SDGs

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akiongea leo katika mkutano muhimu wa ushirikiano wa kimataifa, amesema ikiwa serikali zitaafikiana kwa pamoja malengo ya kumaliza makaa ya mawe, kuongeza ahadi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kuwekeza katika malengo ya dunia, kuna fursa ya kuishinda "changamoto kubwa ya maisha yetu".

Nchi zinazoendelea zaongoza kwa idadi ya watu wenye utipwatipwa

“Katika siku hii ya afya ya mmeng’enyo wa chakula duniani, kwa pamoja tujilotee kushirikiana kutatua tatizo la utipwatipwa kwa mustakabali wa ulimwengu endelevu na wenye afya.” 

Hedhi si ugonjwa, hongera kwa nchi zinazotoa taulo za kike bure- UNFPA 

Leo ni siku ya kimataifa ya hedhi salama ujumbe ukiwa Hatua na Uwekezaji katika Hedhi salama, wakati huu ambapo suala la hedhi linachukuliwa na jamii kuwa ni ugonjwa au mkosi na hivyo kuwakosesha watoto wa kike haki ya kupata huduma ya kujisafi wakati wa mzunguko wa hedhi kila mwezi. 

UNHCR yazindua kampeni ya elimu ya juu kwa wakimbizi vijana 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, leo limezindua kampeni ya kusaka kuwezesha wakimbizi vijana wenye vipaji kuweza kuendelea na elimu ya juu. 

UN yaenzi kujitolea na ujasiri wa walinda amani

Mchango wa vijana katika kuleta amani haupingiki na kuanzia Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC mpaka Lebanon, walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanafanya kazi na vijana kupunguza machafuko na kudumisha amani, ikiwemo upokonyaji wa silaha, kuwakusanya na kuwarejesha tena katika jamii na kuwaingiza katika program za kupunguza machafuko katika jamii.

Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la WHO utumike kuimarisha mifumo ya afya- Guterres 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amehutubia mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Shirika la afya la Umoja wa Mataifa Ulimwenguni, WHO na kusema iwapo ubaguzi katika utoaji chanjo dhidi ya COVID-19 utaendelea, nchi tajiri zitachanja watu wake wote na kufungua chumi zao huku virusi vikiendelea kusambaa na kubadilika katika nchi maskini na kukwamisha mkwamuko wa uchumi ulimwenguni kote. 

Uwekezaji wa mabililioni ya dola dhidi ya COVID-19 utaokoa matrilioni ya dola na maisha- Guterres 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amehutubia mkutano wa masuala ya afya wa viongozi wa kundi la nchi 20 duniani, G20 na kusema kuwa msingi wa kujikwamua vyema kutoka  janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 na kuzuia majanga ya siku za usoni ya kiafya ni kuwepo kwa huduma ya afya kwa wote na mfumo bora wa huduma ya afya ya msingi. 

COVID-19 ikiendelea kutikisa Asia Kusini, UNICEF yataka dola milioni 164 kusaidia kuokoa maisha 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema linahitaji haraka dola milioni 164 ili kuweza kufikisha mitungi ya gesi ya Oksijeni , vipimo vya corona au COVID-19, vifaa tiba kama glovu, vifaa vya kujikinga na vifaa vya kuzuia na kudhibiti maambukizi kwa ajili ya kusaidia kuokoa maisha wakati huu janga la COVID-19 kilishika kasi katikia ukanda mzima wa Asia Kusini. 

Kaya zinazoongozwa na mzazi mmoja zimeongezeka- UN

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya familia, Umoja wa Mataifa unaangazia umuhimu wa teknolojia katika kuimarisha ustawi wa taasisi hiyo muhimu kwa maendeleo endelevu duniani.