Asia Pasifiki

Si haki mtu kupaswa kuchagua kati ya kununua dawa au chakula- Espinosa

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala ulioleta pamoja wadau mbalimbali kujadili kuhusu huduma ya afya kwa wote duniani ikiwa ni maandalizi ya mkutano wa ngazi ya juu wa viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu mada hiyo mwezi Septemba mwaka huu.

Kongamano la kukabiliana na kauli za chuki yafungua pazia Geneva

Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi imefanya kongamano kwa ajili ya kukabiliana na kauli za chuki ili kulinda vikundi vidogo vya kidini, wakimbizi na wahamiaji.

Ubia wa UNHCR na EAA waleta nuru kwa watoto wakimbizi

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandin a muasisi wa taasisi ya Elimu kuzidi vyote, EAA Sheikha Moza bint Nasser wa Qatar, wako nchini Malaysia ambako wameshuhudia jinsi EAA iliyosaidia kuelimisha watoto wakimbizi wa ndani na wale waliotoka nchi jirani.

Hakuna muda wa kusubiri, usugu wa dawa ni janga- Ripoti

Jopo lililoundwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na wadau kubonga bongo kuhusu mbinu bora na endelevu za kukabiliana na usugu wa viuavijiumbe maradhi au antimicrobial limetoa ripoti yake yenye mapendekezo makuu manne kwa lengo la kuondokana na tatizo hilo.

Usalama na afya kazini ni haki ya kila mtu:ILO

Katika kuadhimisha miaka 100 ya shirika la kazi ulimwenguni ILO ambalo dhamira yake ni kuhakikisha ajira bora na zenye hadhi kwa kila mtu, leo ikiwa ni siku ya usalama na afya kazini limetoa wito kwa serikali, waajiri na wafanyakazi kushiriki katika kujenga mazingira salama na yenye afya kazini.

Mpango wa ukanda na mkakati mmoja utakuwa chachu ya kutimiza SDGs:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mpango wa Ukanda na mkakati mmoja unaweza kusaidia kupunguza pengo kubwa la fedha ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

Wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakumbusha msaada wa dharura kwa wakimbizi warohingya Bangladesh

Umoja wa Mataifa umesisitiza ari yake kuendelea kuhakikisha usalama na suluhu ya kudumu kwa wakimbizi warohingya kutoka Myanmar na kukumbusha juhudi za Umoja huo katika kuweka mazingira salama kuwawezesha kurejea nyumbani.

Kutokomeza Malaria kunaanza na mimi- WHO

Leo ni siku ya malaria duniani na shirika la afya ulimwenguni WHO limeungana na nchi na wadau wengine kote duniani kuhimiza vita dhidi ya ugonjwa hatari wa malaria likimtaka kila mmoja kushiriki vita hivyo ili kufikia ajenda afya ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030. 

Watoto zaidi ya milioni 20 wanakosa chanjo ya surua kila mwaka:UNICEF

Takriban watoto milioni 169 kote duniani walikosa chanjo ya kwanza ya dozi ya surua kati ya mwaka 2010 na 2017 , idadi hiyo ikiwa sawa na wastani wa watoto milioni 21.1 kila mwaka , limesema leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Shirika hilo limsema kuongezeka kwa watoto ambao hawajapata chanjo kumechangia milipuko ya surua inayoendelea hivi sasa katika nchi mbalimbali duniani.

Kubebwa muda mrefu, kuendeshwa kwenye vigari na kutumia skrini muda mwingi kwadumaza watoto- WHO

Mwongozo mpya wa shirika la afya  ulimwenguni, WHO unatoa maelekezo ya jinsi ambavyo watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 wanatakiwa kucheza na kufanya shughuli zinazohusisha maungo yao badala ya kubebwa wakati wote au kutumia muda mwingi kwenye skrini za televisheni au michezo yao.