Wakati dunia ikihaha kusaka mbinu za kukabiliana na uchafuzi wa mazingira, sekta ya ubunifu wa mitindo nayo imeshachukua hatua ili kuhakikisha bidhaa zake haziharibu mazingira.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema anatiwa hofu na hatua ya rais wa Sri Lanka ya kuvunja bunge la taifa hilo na kutangaza uchaguzi mpya hapo mwakani.
Kuelekea jukwaa la amani litakaloanza kesho huko Paris, Ufaransa, Rais wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD Gilbert F. Houngbo, amesema atatumia kusanyiko hilo kuwaeleza viongozi wa dunia juu ya umuhimu wa kuwekeza vijijini.
Pengine si wengi wanaoiingia katika mghahawa unaouza mathalani burger yaani nyama iliyofunikwa kwa mkate, wanaowaza kuwa chakula hicho wanachokinunua ni sawa na kushiriki katika kuharibu mazingira. Harakati za binadamu katika kutengeneza nyama ni njia mojawapo za uharibifu unaoacha alama duniani.
Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limetoa wito wa kuhakikisha chakula hakipotei au kutupwa hovyo ili kulinda virutubisho na lishe muhimu kwa ajili ya maisha ya binadamu.
Idadi ya watu waliopoteza maisha wakivuka baharí ya Mediteranea mwaka huu wakienda kusaka hifadhi Ulaya imevuka 2000 baaada ya maiti 17 kupatikana kwenye ufukwe wa Hispania juma hili.
Saudi Arabia imeelezea “kujuta na machungu” kwa mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi, wakati wa mkutano watathimini uliofanyika leo mjini Geneva Uswis na huku ikisisitiza ahadi yake ya kufikia "viwango vya juu zaidi" katika masuala ya haki za binadamu nchini humo, ikiwa ni pamoja na haki za wanawake na wahamiaji.
Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kupunguza athari za majanga, UNISDR, Mami Mizutori amewaeleza wanafunzi wanaokutana katika kongamano la kukuza uelewa kuhusu Tsunami kuwa kupunguza hatari za majanga ni eneo muhimu ambalo linahusu kila taaluma.
Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeingia ushirika na kampuni ya Alibaba, inayoongoza duniani kwa biashara mtandao au E-Commerce, ushirika ambao utasaidia juhudi za kufanikisha lengo namba mbili la maendeleo endelevu SDG la kutokomeza njaa ifikapo mwaka 2030.
Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limezindua mpango utakaowasaidia zaidi ya wakulima 70,000 wa Indonesia pamoja na wafuga wa samaki kuweza kurudia kazi zao za zamani baada ya tetemeko la ardhi na tsunami vilivyosambaratisha mbinu za kukwamua maisha yao.