Asia Pasifiki

Waraka wa siri uliofichuliwa Copenhagen waonyesha mgawanyo wa matarajio kati ya nchi tajiri na zile zenye maendeleo haba

Majadiliano ya Mkutano wa UM juu ya taratibu za kudhibiti bora athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni, Ijumanne yalikabiliwa na mtafaruku na vurugu lisiotarajiwa, baada mataifa yanayoendelea kuonyesha ghadhabu kubwa juu ya waraka wa siri uliofichuliwa na vyombo vya habari,

Mradi wa DOTS wafanikiwa kutibu TB watu milioni 36

Katika miaka 15 iliopita, watu milioni 36 wanaripotiwa walitibiwa, kwa mafanikio, maradhi ya kifua kikuu, au TB, ulimwenguni, kwa kutumia utaratibu mkali wa kuhudumia afya bora uliotayarishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Halijoto duniani, kwa mwongo wa 2000, imefurutu kawaida, imehadharisha WMO

Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) limetangaza ripoti iliobainisha, kihakika, kwamba mwaka 2009 ni miongoni mwa vipindi 10 vilivyoshuhudia kiwango kikubwa kabisa cha halijoto katika dunia, kuanzia 1850, mwaka ambao WMO ulipoanzisha ukusanyaji wa takwimu juu ya kumbukumbu ya halijoto.

Uchina inahimiza nchi tajiri kutimiza haraka ahadi za kupunguza utoaji wa gesi joto na haribifu kwenye anga

Kwa upande mwengine, mjumbe wa Uchina, alitoa mwito maalumu kwa zile nchi zenye maendeleo ya viwanda, unaozihimiza kutimiza, kwa uaminifu, ahadi walizotoa siku za nyuma na kuongoza kwenye kadhi ya kupunguza utoaji wa hewa chafu kwenye anga, kwa viwango vilivyo vikubwa,

Mkuu wa UM kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa, ahimiza wapatanishi kuandaa kidharura marekibisho ya kifedha na kitaaluma kumudu bora athari za gesi chafuzi

Yvo de Boer, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya UM ya Kudhibiti Mabadiliko ya Hali ya Hewa (UNFCCC) kwenye mahojiano aliofanya Ijumanne na waandishi habari, alisema ufunguzi wa Mkutano Mkuu ulianza kwa "hatua ya kutia moyo, na katika nafasi muafaka,

Bidhaa za ndizi, kwenye soko la kimataifa, hazijaathirika na migogoro ya uchumi, imeripoti FAO

Mazao ya ndizi ni bidhaa ya kilimo inayotarajiwa kutoathirika na mizozo ya kifedha, iliotanda karibuni kwenye soko la kimataifa, kwa mujibu wa ripoti iliochapishwa mapema wiki hii na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO).

UNHCR inasema nusu ya wahamiaji duniani huishi mijini

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kwamba zaidi ya asilimia 50 ya wahamiaji milioni 10.5 wanaosaidiwa na taasisi hii ya kimataifa, huwa wanaishi kwenye maeneo ya miji na miji mikuu ya sehemu mbalimbali za dunia.

KM ana matumaini juu ya itifaki ya kupunguza utoaji wa gesi chafu angani

KM Ban Ki-moon kwenye mahojiano na gazeti la kila siku la Denmark, linaloitwa Berlingske Tidende - yaliochapishwa Ijumapili, alisema ana "matarajio ya matokeo mazuri kutokana na majadiliano ya wawakilishi wa kimataifa" kwenye mkusanyiko wa Copenhagen.

UM inahimiza kujumuishwa kwenye miradi ya MDGs mahitaji ya walemavu na walionyimwa uwezo

Kama mlivyosikia kwenye taarifa za habari wiki hii, kwamba Alkhamisi ya tarehe 03 Disemba (2009) iliadhimishwa hapa Makao Makuu ya UM, kuwa ni Siku ya Kimataifa kwa Watu Walemavu na Wenye Kunyimwa Uwezo wa Kimaumbile.

Mkutano wa Cartagena umepitisha azimio la kukomesha mateso ya silaha zilizotegwa

Kwenye Mkutano Mkuu wa Mapitio juu ya Ulimwengu Huru dhidi ya Silaha za Mabomu Yaliotegwa Ardhini, unaofanyika kwenye mji wa Cartagena, Colombia, Mataifa Wanachama yalioidhinisha na kuridhia Mkataba wa Kupiga Marufuku Mabomu Yaliotegwa, yameahidi tena kukomesha usumbufu na madhara yanayoletwa na silaha hizo.