Asia Pasifiki

Baraza la Usalama

Alkhamisi Baraza la Usalama asubuhi lilianza shughuli zake kwa kujadilia hali katika Cyprus, na maendeleo kuhusu mazungumzo ya kusawazisha mfarakano baina ya raia wa Kigiriki na wale wa Kituruki.

Takwimu mpya za WHO juu ya maambukizi ya vimelea vya H1N1

Dktr Keiji Fukuda, Mkurugenzi Mkuu Mwandamizi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kwenye mahojiano Alkhamisi na waandishi habari mjini Geneva, alitangaza takwimu mpya juu ya maambukizo ya homa ya mafua ya nguruwe, ambayo kuanzia leo itajulikana rasmi kama homa ya vimelea vya H1N1.

Orodha ya wagombea wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu yatangazwa rasmi na IAEA

Shirika la UM Kuhudumia Matrumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) limetangaza kuwa limepokea orodha rasmi ya wagombea uchaguzi wa cheo cha Mkurugenzi Mkuu mpya wa taasisi hii ya kimataifa baada ya kiongozi wa sasa Mohamed ElBaradei kutangaza atastaafu atakapomaliza muda wake mwaka huu.

Nchi saba zimegundua waathirika wa homa ya mafua ya nguruwe, WHO imethibitisha

Mkurugenzi wa Taasisi ya Marekani ya Kudhibiti Maradhi (CDC) amenakiliwa na vyombo vya habari akithibitisha ripoti inayosema mtoto mchanga wa miezi 23, katika jimbo la Texas, amesajiliwa kufariki kufuatia maambukizo ya homa ya mafua ya nguruwe. Kifo hiki ni cha kwanza kutukia Marekani, miongoni mwa wale watu waliopatwa na ugonjwa huo.

Siku ya kuwakumbuka waathirika wa silaha za kemikali

KM wa UM Ban Ki-moon ameyasihi Mataifa Wanachama kuchukua hadhari kuu ili kuhakikisha silaha maututi za kemikali hazitodhibitiwa katu na makundi ya magaidi. KM aliyasema haya kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kuwakumbuka Waathirika wa Mapigano Yanayotumia Kemikali.

Makampuni ya madawa yanahimizwa na IAEA kuunda chombo rahisi kudhibiti saratani

Shirka la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) limeyahamasisha makampuni yanayotengeneza vifaa na zana za matibabu kuunda chombo kipya cha tiba ya saratani kkitakachokuwa na nguvu, chepesi, kinachobebeka, rahisi kutumia na ambacho watu wa kawaida watamudu kukinunua.

ILO kuwakumbuka waliojeruhiwa na kuuawa kwenye mazingira ya vibarua

Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) limeripoti tarehe 28 Aprili itaadhimishwa kuwa ni Siku ya Usalama na Afya ya Ajira Duniani. Mataifa Wanachama kadha pamoja na mamia ya sehemu mbalimbali za dunia, yatashiriki kwenye taadhima za kuihishimu siku hiyo, zikijumlisha kumbukumbu maalumu za wafanyakazi waliojeruhiwa au kufariki wangali wakiendeleza majukumu ya vibarua walivyoajiriwa.

WHO inahadharisha homa ya nguruwe inahatarisha kuenea kimataifa kama haijadhibitiwa mapema

Dktr Margaret Chan, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Afya Duniani (WHO) kwenye mahojiano na waandishi wa habari mwisho wa wiki [25/04/2009], alihadharisha mripuko wa karibuni wa aina ya virusi vya homa ya mafua - inayotambuliwa kwa umaarufu kama homa ya mafua ya nguruwe - katika maeneo ya Mexico na Marekani, inatakikana kudhibitiwa mapema, au si hivyo homa hii inaashiriwa itaenea kwa kasi na kudhuru fungu kubwa la umma wa kimataifa.

Mkutano juu ya Mwito wa Durban Kupinga Ubaguzi wahitimishwa Geneva

Mkutano wa Mapitio juu ya Mwito wa Durban dhidi ya Ubaguzi, uliofanyika wiki hii mjini Geneva, Uswiss ulikamilisha shughuli zake leo Ijumaa. Kwenye mahojiano na waandishi habari wa kimataifa juu ya kikao hicho, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Bindamau, Navi Pillay alisema anaamini Mkutano ulikuwa wa mafanikio makubwa, licha ya kwamba mapatano yalikuwa magumu na yalichukua muda mrefu kukamilishwa.

Bei kuu ya chakula katika nchi masikini inaendelea kutesa mamilioni, kuhadharisha FAO

Kwenye ripoti iliotolewa na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) - yenye mada isemayo ‘Hali ya Chakula na Matarajiao ya Baadaye ya Mavuno\' - ilieleza kwamba bei ya juu ya chakula katika mataifa yanayoendelea inaendelea bado kusumbua na kuwatesa mamilioni ya umma masikini, raia ambao tangu mwanzo umeathirika na matatizo sugu ya njaa na utapiamlo, licha ya kuwa mavuno ya nafaka ulimwenguni, kwa ujumla, yameongezeka katika kipindi cha karibuni, na bei za chakula ziliteremka kimataifa, hali kadhalika.