Asia Pasifiki

COVID-19 imekwangua vipato kwa familia zenye watoto- Ripoti

Tangu kuanza kwa janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 mwaka 2020, kaya mbili kati ya tatu duniani kote zenye watoto zimepoteza vipato, imesema ripoti mpya iliyochapishwa leo na Benki ya Dunia na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF. 

Thamani ya mchango wa wanawake haielezeki, bila ujumuishwaji wao hakuna maendeleo:UN

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake hii leo Umoja wa Mataifa umehimiza kuthamini mchango wao na kuwajumuisha katika kila nyanja ili kutimiza ajenda ya maendeleo endelevu na kukabili changamoto zingine zikiwemo janga la COVID-19 na mabadiliko ya tabianchi. 

Kote duniani wanyamapori wako hatarini – Antonio Guterres

“Kwa kuharibu ulimwengu wa asili, tunatishia ustawi wetu wenyewe.” Amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake wa siku ya wanyamapori inayoadhimishwa leo.

Tuwajali wavuvi wadogo wadogo – FAO

Mkutano wa siku nne wa wakuu wa nchi zenye bahari duniani, unaanza leo huko Roma Italia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limetoa wito kwa wasomi, serikali, mashirika ya kiraia na sekta binafsi kutambua umuhimu wa wavuvi wadogo wadogo na ufugaji wa samaki, ambao ni sehemu muhimu ya uvuvi.

Kuwajengea vyoo watoto wenye ulemavu kumewaimarisha kisaikolojia : UNICEF

Kambi ya wakimbizi ya Za'atari nchini Jordan inakadiriwa kuwa mtoto 1 kati ya 10 ana ulemavu, na idadi hiyo huwa kubwa zaidi wakati wa dharura.

FAO yapatia wakulima Afghanistan mbegu bora za kuhimili ukame

Msimu wa upanzi wakati wa majira ya chipukizi ukiwa unakaribia huko nchiin Afghanistan, shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limepatia wakulima mgao wa mbegu bora za ngano ili kuepusha njaa ilIyowakumba mwaka jana kutokana na kuchelewa kupanda mbegu bora wakati wa msimu wa baridi kali. 
 

Anga ndio paa letu na ardhi ndio zulia letu, alalama mkimbizi Afghanistan

Nchini Afghanistan, majira ya baridi kali yamebisha hodi huku wakimbizi wa ndani waliosaka hifadhi kwenye mji mkuu Kabul wakihaha kujikinga na familia zao kwenye mahema yasiyo na vifaa vya kuleta joto, watoto, wanawake na wanaume wakiwa hatarini. 
 

Fahamu mambo ya kufanya kutokomeza saratani  ya shingo ya kizazi

Ikiwa mwezi huu wa Januari ni mwezi wa kuelimisha kuhusu saratani ya shingo ya kizazi, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema saratani hiyo inaweza kuwa ina ya kwanza ya saratani kutokomezwa ulimwenguni iwapo serikali itaongeza huduma za tiba na kinga.

Kilimo cha uyoga chakomboa familia nchini Bangladesh

Mafunzo ya kilimo cha kisasa cha uyoga na msaada wa kutafutia wakulima masoko ya zao hilo yanayotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP yameleta nuru kwa wakulima nchini Bangladeshi akiwemo Sahera Begum ambaye anasema uyoga umemkomboa yeye na familia yake. 

Chanjo chanjo chanjo ndio jawabu mujarabu dhidi ya Omnicron- WHO

Virusi aina ya Omnicron vikiendelea kuwa sababu ya kasi kubwa ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona au COVID-19 hivi sasa duniani kote, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO hii leo limesema ni muhimu hatua zaidi zikachukuliwa ili kusaidia nchi zote kupata haraka iwezekanavyo chanjo dhidi ya Corona kwa kuwa ndio mkombozi iwapo mtu anaambukizwa na tayari ana chanjo.