Shirika la afya ulimwenguni, WHO limetoa mwongozo na mbinu za kuwezesha viongozi kwenye maeneo ya majiji kuweza kukabiliana na visababishi vikuu vya vifo kwenye maeneo hayo.
Zaidi ya nusu ya idadi ya watu duniani hivi sasa wanaishi mijini na kufikia mwaka 2050 theluthi mbili ya watu watakuwa wanaishi mjini na makazi ya kuendana na ongezeko la watu bado hayajakarabatiwa na miji mipya itahitaji kujengwa.
Rais wa mfuko wa maendeleo ya kilimo wa Umoja wa Mataifa Gilbert Houngbo akiwa ziarani India ametembelea miradi ya IFAD inayowawezesha wanawake wa vijijini nchini India.
Utafiti mpya wa shirika la afya ulimwenguni, WHO, umebaini kuwa theluthi mbili ya wanawake wenye uwezo wa kubeba mimba na ambao wana nia ya kuchelewesha kupata ujauzito au kudhibiti idadi ya watoto huacha kutumia huduma za uzazi wa mpango kwa hofu ya madhara ya huduma hizo.
Ripoti mpya ya shirika la afya duniani, WHO, imesema kuwa watu wengi zaidi walipata tiba dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu, TB, mwaka 2018 kuliko wakati wowote ule kutokana na kuimarika kwa mbinu za utambuzi wa ugonjwa huo.
Taasisi ya kimataifa ya utafiti wa saratani, IARC na wadau wake wamezindua toleo la tatu la atlasi au kitabu cha ramani kinachoonesha hali ya saratani duniani.
Idadi kubwa ya watoto wanateseka kutokana na lishe duni na mifumo ya chakula ambayo inawadumaza, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika ripoti kuhusu hali ya watoto duniani kwa mwaka huu wa 2019 ikiangazia zaidi watoto, chakula na lishe.
Katika kuelekea siku ya chakula duniani ambayo kila mwaka hufanyika Oktoba 16, shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, limesema kila mwaka theluthi moja ya chakula kinachozalishwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu kina pote bure au kutupwa. Maelezo zaidi na Flora Nducha
Utafiti mpya wa Shirika la afya ulimwenguni, WHO, unaonesha kwamba theluthi moja ya wanawake katika nchini 4 za kipato cha chini wameripoti kukumbwa na mateso wakati wa kujifungua.
Takribani watu bilioni 2.2 duniani kote wana uoni hafifu au upofu, kutokana na ukosefu wa huduma bora za afya, limesema shirika la afya duniani, WHO, hii leo katika ripoti yake ya kwanza kuhusu hali ya uoni duniani.