Zaidi ya nusu ya watoto wakimbizi milioni 7.1 wa umri wa kwenda shule hawaendi shule, ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR iliyotolewa leo imebainisha. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema mataifa ya Afrika yanaweza kunufaika zaidi kutokana na ufahamu na utamaduni wa Japani katika ulaji wa vyakula vyenye afya na lishe, amesema Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Qu Dongyu.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye yuko Biarritz Ufaransa kushiriki mkutano wa kundi la nchi 7 zenye uchumi wa juu zaidi duniani, G7, ametumia fursa hiyo kuendelea kupaza sauti ya udharura wa mabadiliko ya tabianchi unaokumba ulimwengu hivi sasa.
Utafiti zaidi na maendeleo katika vifaa vya kuzuia malaria na tiba ni muhimu ili kutokomeza malaria katika siku zijazo limesema shirika la afya ulimwenguni, WHO leo Ijumaa kupitia ripoti yake iliyozinduliwa Geneva Uswisi.
Chembechembeza plastiki ziko kila sehemu lakini havihatarishi afya ya binadamu limesema Shirika la afya ulimwenguni, WHO leo Alhamisi. Grace Kaneiya na maelezo zaidi.
Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuadhimisha waathirika wa matendo ya vurugu yanayotokana na dini au imani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ulimwengu unapaswa kupinga na kukataa wale ambao kwa mabavu na kwa uongo wanashawishi kujenga imani potofu, kuchochea mgawanyiko na kueneza hofu na chuki.
Shirika la chakula na kilimo duniani FAO limeonyesha mfano wa manufaa yanayoanza kupatikana kutokana na matumizi mbadala ya bidhaa za plastiki, ikiwemo vifungashio ambavyo hivi sasa kampuni zinatengeneza ili kupunguza matumii ya vifungashio vya plastiki vinavyochafua mazingira.
Ardhi ni rasilimali muhimu ambayo iko katika shinikizo kubwa kutoka kwa binadamu na mabadiliko ya tabia nchi, lakini pia inaweza kuwa sehemu ya suluhu ya changamoto hizo imesema ripoti ya jopo la kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi IPCC.
Tume huru ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa nchini Myanmar imeitaka jumuiya ya kimataifa kukata uhusiano na jeshi la Myanmar na mtandao mkubwa wa makampuni linayoyathibiti na kuyategemea na kuliwekea vikwazio vikiemo vya silaha.
Sera zilizo rafiki kwa masuala ya familia ni muhimu katika kuhakikisha idadi ya watoto wachanga wanaonyonyeshwa katika miezi sita ya mwanzo ya maisha yao inaongezeka kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF.