Mapigano makali yameendelea leo asubuhi kwenye eneo la Ghouta Mashariki nchini Syria licha ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kutaka sitisho la mapigano kwa siku 30 ili misaada ifikie wahitaji na wagonjwa waweze kuhamishwa.
Wabunge kutoka nchi mbalimbali duniani wanakutana makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani kubadilisha mawazo ya jinsi ya kukabiliana na suala mtambuka la uhamiaji.