Katika siku ya kimataifa ya kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashata ya utumwa katika bahari ya Atlantiki hii leo Katiku Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema ili kuwaenzi vyema mamilioni ya watu wenye asili ya Afrika waliopitia madhila asiyoelezeka katika utumwa na biashara ya utumwa ni vyema kuyania wazi yaliyowasibu na kuhakikisha yatokomezwa
Idadi ya wagonjwa wa COVID-19 imeendelea kuongezeka kote dunini kwa wiki ya nne mfululizo huku wagonjwa milioni 3.3 wapya wakiripotiwa katika siku saba zilizopita limesema leo shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO.
Katika kuadhimisha siku ya utabiri wa hali ya hewa duniani hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amesema hali ya hewa na maji havitengamani na kimoja hakiwezi kuwepo bila kingine vivyo hivyo katika maisha ya binadamu.
Mfuko wa kimataifa wa mshikamano wa kukabiliana na janga la corona au COVID-19 leo umeadhimisha mwaka mmoja tangu kuzinduliwa na kutoa ombi la kuendelea kutunishwa ili kuwasaidia wahitaji wengingi zaidi wakati huu janga likiendelea kuitikisa dunia.
Ripoti ya tathimini mpya iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF imeonya kwamba huenda kukawa na ndoa zingine za utotoni milioni 10 kabla ya kumalizika kwa muongo huu na hivyo kutishia miaka ya hatua zilizopigwa katika kupunguza ndoa hizo.
Pato la msingi la muda mfupi (TBI) likitolewa kwa mamilioni ya wanawake katika nchi zinazoendelea duniani linaweza kuzuia kuongezeka kwa umasikini na kupanuka kwa pengo la usawa wa kijinsia wakati huu wa janga la corona au COVID-19, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Leo dunia inaadhimisha siku ya usikivu wa masikio katika kipindi ambacho tayari ripoti mpya ya shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO imetahadharisha kuwa kufikia mwaka 2050 takribani watu bilioni 2.5 ulimwenguni watakuwa wanaishi na kiwango fulani cha kupoteza uwezo wao wa kusikia ikiwa hatua hazitachukuliwa mapema.
Misitu ni uhai na sio tu kwa binadamu na mazingira bali pia kwa asilimia 80 ya viumbe vyote vya porini, hivyo kutumia vyema na kuilinda ni kwa maslahi ya watu wote, sayari dunia na maendeleo amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku ya wanyamapori duniani inayoadhimishwa leo.