Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hilary Clinton akizungumza kwenye mkutano wa baraza la haki za binadamu amesema macho yote hii leo yanajikita kwa Libya.
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limesema kuwa uwekezaji wa kiasi cha dola za kimarekani bilioni 1.2 kwa watoto wenye umri kati ya miaka 10 hadi 19 kunaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza wigo wa umaskini.
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza alhamisi hii muhula wa kuwepo vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Timor ya Mashariki kwa mwaka mmoja.Tume hii inayojulikana kama UNMIT itafanya kazi hadi tarehe 26 mwezi februari mwaka wa 2012.
Akitumia karata ya tuzo ya Oscar iliyotwaa Umoja wa Mataifa miaka 60 iliyopita kupitia filamu iliyoelezea hali ngumu za watoto wenye ulemavu, Katibu Mkuu Ban Ki-moon ameanza kuishawishi Hollywood ili kukusanya fedha na hatimaye kuisambaza filamu hiyo duniani kote.
Mjumbe huyo amesema kuwa kukosoa jambo siyo dhambi wala uchochezi hivyo mamlaka lazima zitambue kwamba wakosoaji wa haki za binadamu wanafanya hivyo kama njia ya kujenga jamii adilifu na yenye kuheshimu misingi ya kibinadamu.
Mwanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan amesema kuwa hali ya usalama katika nchi hiyo bado ni ya kiwango cha chini ambayo imechochewa na kuondolewa madarakani kwa utawala wa Taliban mwaka 2001.
Wananchi wa taifa la Timor-Leste hatimaye wameingia kwenye duru mpya ya mashikamano na maendeleo na kuiaga enzi ya machafuko na mizizo iliyokumba eneo hilo kwa miaka mingi.