Asia Pasifiki

Joto laendelea kuongezeka duniani kwa mwaka wa 7 mfululizo: WMO 

Viashiria vinne vinavyotumika kupima hali ya hewa duniani vyote vimeonesha hali kuendelea kuwa mbaya duniani licha ya wadau kila uchwao kujadiliana na kuahidi kuchukua hatua madhubuti za kulinda dunia kutoathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi ambayo kwakiasi kikubwa wanaathiriwa na shughuli za kibinadamu.

Joto laendelea kuongezeka duniani kwa mwaka wa 7 mfululizo: WMO

Viashiria vinne vinavyotumika kupima hali ya hewa duniani vyote vimeonesha hali kuendelea kuwa mbaya duniani licha ya wadau kila uchwao kujadiliana na kuahidi kuchukua hatua madhubuti za kulinda dunia kutoathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi ambayo kwa kiasi kikubwa wanaathiriwa na shughuli za kibinadamu. 

Fikra potofu kuhusu mimba zisizotarajiwa -Sehemu ya kwanza

Nusu ya ujauzito ambao wanawake na wasichana wanabeba si wao wameamua. Hili ni janga ambalo limepuuzwa. Imesema UNFPA, ambalo ni shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi kupitia ripoti yake ya hali ya Idadi ya Watu Duniani kwa mwaka huu wa 2022. 

Ripoti mpya ya UNICEF yaonya kuhusu tatizo la uzito mdogo kwa watoto  

Idadi ya watoto walioathirika na uzito mdogo wa kupindukia imekuwa ikiongezeka hata kabla ya vita ya Ukraine ambayo inatishia kuitumbukiza dunia kwenye mgogoro mkubwa wa chakula imeonya ripoti mpya kuhusu watoto iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Fifisha mwanga wa taa usiku ili kuokoa maisha ya ndege wanaohama duniani:UN 

Katika siku ya ndege wanaohama duniani Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuchukua hatua kufifisha nuru ya mwanga usiku ili kunusuru maisha ya mamilioni ya Ndege kila mwaka. 

Muungano mpya wazinduliwa kuhakikisha lishe bora kwa watoto na kila mtu: UN

Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani WHO, la kuhudumia Watoto UNICEF, la mpango wa chakula duniani WFP na la mazingira UNEP leo yamezindua muungano mpya kwa lengo la kuchukua hatua ili kuhakikisha lishe bora kuanzia mifumo endelevu ya chakula kwa watoto na kila mtu. 

G7: FAO yatoa mapendekezo ya kukabiliana na uhaba wa chakula wa sasa na ujao

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO Qu Dongyu ametoa wito kwa nchi tajiri zaidi duniani G7 kusaidia kukabiliana na uhaba wa chakula katika siku zijazo kwani vita inayoendelea nchini Ukraine imepunguza usambazaji na kupandisha bei juu katika viwango vya kuvunja rekodi na kuyaweka mashakani mataifa ambayo tayari yana hatari ya kuathirika kote barani Afrika na Asia.

Siku ya kimataifa ya Afya ya mimea yaadhimishwa kwa mara ya kwanza 

Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Afya ya Mimea, IDPH, ulimwengu ukiadhimisha siku hiyo kwa mara ya kwanza, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, limesema mabadiliko ya tabianchi na shughuli za binadamu zinabadilisha mifumo ikolojia na kuharibu bayonuai huku hali hiyo ikiunda maeneo mapya kwa ajili ya wadudu waharibifu kustawi.  

Kampeni ya ‘Be Seen Be Heard’ yaani ‘Onekana Sikika’ yazinduliwa kuwapa sauti vijana ulimwenguni 

Vijana wana haki ya kujumuishwa katika maamuzi ya kisiasa yanayowahusu, hata hivyo, vikwazo vingi vinazuia ushiriki wao. 

Hali mbaya ya kiuchumi Sri Lanka: Bachelet anahimiza mazungumzo ili vurugu zisiongezeka

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Michelle Bachelet ametoa wito kwa mamlaka nchini Sri Lanka kuzuia ghasia zaidi na kushiriki mazungumzo ya kushughulikia malalamiko ya wananchi kufuatia mzozo mkubwa wa kiuchumi nchini humo.