Asia Pasifiki

Uwazi katika bidhaa za chakula ni muhimu: FAO

Uwazi katika soko la bidhaa za chakula ni muhimu sana wakati huu ambapo dunia inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa chakula kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo Vita, mabadiliko ya tabianchi na kupanda kwa bei za chakula.

Uwazi wa teknolojia kwenye sayansi utanufaisha dunia nzima: WHO

Baraza la wataalamu wa Sayansi la Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limetoa ripoti yake ya kwanza likitaka kuwepo na usawa wa kupatikana teknolojia ya kusoma vinasaba au Genomics baina ya nchi tajiri na zile zinazoendelea duniani. 

Habari za uongo, upotoshaji na matamshi ya chuki vinatumika kama silaha za vita: Guterres

Umoja wa Mataifa - UN umesema umeimarisha mawasiliano ya kimkakati katika operesheni za ulinzi wa amani duniani kote ili kukabiliana na taarifa za upotoshaji au uongo zinazoenezwa hususan mitandaoni.  

Tumieni chanjo zilizopo kukabiliana na viua vijiumbe maradhi: WHO

•    WHO yataka chanjo zilizopo sasa zitolewa kimataifa kwa usawa
•    WHO yataka uharakishwaji wa mchakato wa upatikanaji wa chanjo
•    Utengenezaji wa chanjo uharakishwe kama ilivyokuwa kwenye chanjo za COVID19

WHO yatoa mwongozo mpya kwa wagonjwa wa kifua Kikuu

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO hii leo limetoa kitabu kipya cha mwongozo kilicho sheheni maelekezo pamoja na sura mpya kadhaa za namna ya kuwahudumia wagonjwa wa Kifua kikuu au TB lengo likiwa ni kuboresha maisha yao pamoja na kuwapa matokeo bora ya kitabibu.  

Umoja wa Mataifa uko tayari kuisaidia Sri Lanka na watu wake – Katibu Mkuu UN 

“Katibu Mkuu anaendelea kufuatilia kwa karibu yanayoendelea nchini Sri Lanka.” Imeeleza taarifa kutoka Ofisi ya Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo Jumatatu. 

Mauaji na utekaji nyara wa watoto kwenye maeneo ya vita vilishamiri mwaka 2021- Ripoti

Mwaka wa 2021  umeshuhudia mchanganyiko wa mwendelezo hatari wa mizozo, mapinduzi ya kijeshi sambamba na mizozo mipya na ile iliyodumu muda mrefu na ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa, vyote ambavyo kwa pamoja vimekuwa na madhara makubwa kwa watoto duniani kote, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ripoti yake ya mwaka kuhusu Watoto kwenye mizozo ya kivta, ripoti ambayo imechapishwa hii leo.

Nimesikitishwa sana na mauaji ya kutisha ya Shinzo Abe – António Guterres 

Muda mfupi baada ya Japan kutangaza kifo cha Waziri Mkuu wake wa zamani, Shinzo Abe, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ameeleza kusikitishwa sana na mauaji hayo ya kutisha. 

Mabadiliko ya tabianchi na majanga mengine yaweka njiapanda SDGs:UN

Ripoti mpya ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs kwa mwaka 2022 iliyotolewa leo na Umoja wa Mataifa imesema mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi, janga la COVID-19 na ongezeko la idadi ya migogoro na vita kote duniani vimeyaweka malengo yote 17 ya maendeleo endelevu njiapanda.

Wagonjwa wa COVID19 na Monkeypox waongezeka duniani

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limehimiza nchi wanachama kuhakikisha zinaendelea  kujikinga na janga la COVID19 kwakuwa janga hilo lingalipo na takwimu za wiki mbili zilizopita zinaonesha kuongezeka kwa wagonjwa kwa takriban asilimia 30.