Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na UKIMWI -UNAIDS, umekaribisha mchango wa nyongeza wa zaidi ya dola 977,000 kwa ajili ya harakati zake za kupambana na ugonjwa huo.
Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamesema hatua za haraka zinahitajika ili kuondokana na tabia inayotishia mafanikio ya haki za wanawake duniani yaliyopatikana kwa jasho.
Kuendelea kushika kasi kwa msimu wa pepo kali na mvua za monsoon kumeongeza shinikizo la mahitaji ya kiafya kwamaelfuya wakimbiz wa Rohingya walioanza kumiminika nchini Bangladesh kwa wingi yapata miezi 10 iliyopita.
Muonekano wa dunia ukiwa katika mamia ya kilometa kutoka anga za mbali unavutia sana amesema Scott Kelly kinara wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya anga , ambaye pia ni mwanaanga wa zamani wa Marekani.
Watu milioni 68.5 walikuwa wamefurushwa kutoka makwao hadi mwishoni mwa mwaka 2017, imesema ripoti mpya ambayo imetolewa leo huko Geneva, Uswisi na shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR.
Shirika la fedha duniani, IMF halina maadili ya kutosha ya kuweza kulinda mataifa ya kipato cha chini, amesema mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu umaskini uliokithiri na haki za binadamu.
Mataifa ni lazima yachukue hatua kukomesha unyanyapaa ulioenea na wa kitaasisi unaoelekezwa kwa watu walio na ukoma pamoja na familia zao, amesema mtaalam maalum kuhusu utokomezaji wa unyanyapaa dhidi ya watu walio na ukoma na familia zao, Alice Cruz.