Amerika

Hapa na Pale

Uturuki umekabidhiwa uraisi wa duru wa Baraza la Usalama kwa mwezi Juni, baada ya Shirikisho la Urusi kukamilisha uongozi wa shughuli za Baraza kwa mwezi Mei. Wajumbe wa Baraza la Usalama watakutana Ijumanne asubuhi kuzingatia mpango wa kazi na ajenda ya mikutano ya mwezi Juni. Baada ya hapo, Balozi Baki Ilkin wa Uturuki atafanya mazungumzo na waandishi habari wa kimataifa wa Makao Makuu, kuelezea masuala yatakayopewa umuhimu kwenye mijadala ya Baraza la Usalama chini ya uongozi wa Uturuki.

Mazungumzo ya kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa yaanza rasmi Bonn

Duru ya pili ya Mazungumzo ya UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani imeanza rasmi majadiliano Ijumatatu ya leo, kwenye mji wa Bonn, Ujerumani ambapo kutazingatiwa, kwa mara ya kwanza, waraka wa ajenda iliofikiwa na nchi wanachama karibuni, ya kudhibiti bora taathira za mageuzi ya mazingira yanayoletwa na hali ya hewa ya kigeugeu.

Mtumishi wa UM kutoka Tanzania anazungumzia maana halisi ya "Sikukuu ya Walinzi Amani wa Kimataifa" pamoja na mchango wa wanawake

Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya UM imeandaa kipindi maalumu kuiadhimisha \'Sikukuu ya Walinzi Amani wa Kimataifa\' kwa 2009, makalailiokusudiwa kubainisha mchango wa vikosi vya wanajeshi, polisi na watumishi raia katika kuimarisha utulivu na amani duniani.

Siku ya kimataifa dhidi ya matumizi ya tumbaku- 31 Mei 2009

Tarehe 31 Mei, ambayo mwaka huu itaangukia Ijumapili, huadhimishwa kila mwaka na UM, kuwa ni Siku ya Upinzani Dhidi ya Matumizi ya Tumbaku Ulimwenguni.

UM waadhimisha 'Sikukuu ya Kuwakumbuka Walinzi Amani wa Kimataifa'

Siku ya leo, tarehe 29 Mei (2009) inaadhimishwa na UM kuwa ni ‘Siku Kuu ya Kumbukumbu ya Walinzi Amani wa Kimataifa.’

ILO inatabiri kukithiri kwa wasiyekuwa na kazi duniani katika 2009

Juan Somavia, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) amewasilisha ripoti mpya, kwa kupitia Geneva, yenye kutabiri idadi ya watu wasiyekuwa na kazi mwaka huu, itaongezeka kwa kima cha baina ya watu milioni 39 hadi milioni 59.

Utabiri wa DESA juu ya hali ya uchumi duniani kwa 2009

Idara ya UM juu ya Masuala ya Kiuchumi na Jamii (DESA) asubuhi iliwasilisha rasmi, ripoti ya katikati ya mwaka, yenye mada isemayo “Hali ya Uchumi Duniani na Matumaini kwa 2009”. Ripoti ilibashiria uchumi wa ulimwengu kwa mwaka huu utateremka kwa asilimia 2.6, baada ya huduma za kiuchumi kupanuka kwa asilimia 2.1 katika 2008, na baada ya kupanuka, vile vile, kwa karibu asilimia 4 kila mwaka katika kipindi cha baina ya 2004 na 2007.

Mkutano wa BK kuzingatia matatizo ya uchumi na fedha duniani waakhirishwa

Ijumanne asubuhi, kwenye kikao cha wawakilishi wote wa Baraza Kuu (BK) la UM, kulichukuliwa uamuzi wa pamoja wa kuakhirisha Mkutano Mkuu juu ya Migogoro ya Uchumi na Fedha Duniani na Athari Zake Dhidi ya Maendeleo, kikao ambacho kilitarajiwa kifanyike baina ya Juni 1 hadi 03.

Mashirika ya afya yanaomba kufadhiliwa misaada ziada kupambana na homa ya manjano

Mashirika ya UM juu ya maendeleo ya watoto, UNICEF, na afya, WHO, yameonya kwamba akiba ya dharura ya chanjo dhidi ya homa ya manjano katika Afrika imo hatarini ya kumalizika mwaka ujao, kwa sababu ya upungufu wa misaada ya kufadhilia uzalishaji wa dawa hizo kutoka wahisani wa kimataifa.