Amerika

UNODC inajiandaa kutangaza ripoti ya 2009 juu ya tatizo la madawa ya kulevya duniani

Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC) litawakilisha Ijumatano ripoti mpya kuhusu tatizo la madawa ya kulevya ulimwenguni katika 2009.

Mkuu wa UN-HABITAT atunukiwa "Tunzo ya Goteberg"

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Makazi (UN-HABITAT), Anna Tibaijuka, ametangazwa kuwa ni mmoja wa washindi watatu wa Tunzo ya Göteberg, kwa michango yao ya kitaifa na kimataifa, katika maamirisho ya huduma ya maendeleo yanayosarifika.

Afya ya wahamiaji dhidi ya UKIMWI inazingatiwa na bodi la UN-AIDS,linalokutana rasmi Geneva

Bodi la la Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya UKIMWI (UNAIDS) limeanza rasmi Geneva kikao cha 24, kilichokusudiwa kuzingatia mahitaji ya umma unaohama hama, ukijumuisha wahamaji na wahamiaji wa ndani na nje ya mataifa yao.

Ripoti ya kisayansi kuonya walimwengu, mabadiliko ya hali ya hewa duniani sio mzaha

Wataalamu wa kimataifa wa katika fani ya sayansi, juzi waliwasilisha ripoti mpya yenye kusisitiza kwamba mabadiliko ya hali ya hewa, yalioripotiwa kujiri kimataifa katika miaka ya karibuni, ni matukio hakika kwenye mazingira na sio mnong’ono wala makisio.

Siku Kuu ya Wahamiaji Duniani 2009

Ijumamosi ya tarehe 20 Juni 2009, itahishimiwa rasmi na UM kuwa ni ‘Siku ya Wahamiaji Duniani\'. Kaulimbiu ya mwaka huu inasema "Mahitaji Hakika, kwa Umma Halisi".

Mkutano wa kudhibiti athari za maafa wapendekeza vifo vipunguzwe kwa nusu 2015

Mkutano wa Kimataifa Kupunguza Hatari Inayoletwa na Maafa umemalizika mjini Geneva leo Ijumaa, ambapo kulitolewa mwito maalumu unaowataka viongozi wa kisiasa katika Mataifa Wanachama kuchukua hatua za dharura kupunguza, angalaukwa nusu idadi ya vifo vinavyosababishwa na maafa ya kimaumbile itakapofika 2015, .

Idadi ya wenye njaa kukiuka bilioni 1 duniani katika 2009, inasema FAO

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limetangaza jumla ya watu waliopo kwenye ukingo wa kubanwa na matatizo ya njaa ulimwenguni katika 2009, inakaribia watu bilioni 1.02 - sawa na sehemu moja ya sita ya idadi nzima ya watu duniani.

Kilimo hujiokoa zaidi na mizozo ya kiuchumi kushinda sekta nyenginezo, inasema ripoti ya FAO/OECD

Ripoti ya pamoja iliotolewa na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD), iliowakilishwa rasmi Ijumatano, imeeleza kwamba ilivyokuwa uchumi wa kimataifa hautarajiwi kufufuka na kuota mizizi ya kuridhisha mpaka baada ya miaka miwili/mitatu ijayo, wataalamu wanaashiria mporomoko wa muda wa bei za bidhaa za kilimo kimataifa utakuwa wa wastani.

Wanariadha wa kimataifa kushiriki kwenye miradi ya kupiga vita njaa ulimwenguni

Jarno Trulli na Timo Glock, madereva wa mashindano ya mbio za gari, wenye kuwakilisha kampuni za Panasonic na Toyota, wanatazamiwa kuvalisha na kupamba gari zao na alama ya kitambulisho ya lile Shirika UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP), pale watakaposhiriki kwenye mashindano ya gari Uingereza mnamo Ijumapili ijayo.

WHO-UNICEF yasisitiza jitihadi kuu zahitajika kuhifadhi mahospitali na skuli penye maafa

Mashirika ya UM juu ya afya na maendeleo ya watoto, yaani mashirika ya WHO na UNICEF, yametoa mwito wa pamoja wenye kuzihimiza serikali za kimataifa, kuchukua hatua madhubuti, katika sehemu nne muhimu zinazohitajika kupunguza athari za maafa katika mahospitali na maskuli.